Monday, October 31, 2011

PICHA "MBAYA" ZA BI HARUSI MTARAJIWA ZANASWA

Picha  za Bi Harusi mtarajiwa ambaye ni modal sexy Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ hivi karibuni zimenaswa akiwa katika mapozi ya kimahaba na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Martin.

Picha hizo ambazo zipo kwenye mtandao zinawaonesha wawili hao wakijiachia kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, mazingira yaliyosababisha baadhi ya watu kuhoji juu ya ukaribu wao huo
 Katika kujua uhusiano uliopo kati ya wawili hao, mpekuzi wetu alimtafuta Jack kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana mara moja.

Martin alipopatikana alisema: “Picha hizo tulizipiga siku tuliyokuwa tunaandaa matangazo flani hivi, ila hazina maana yoyote mbaya, Jack ni mshikaji wangu wa kawaida tu.”

 
Jack ambaye ni Miss Ilala namba 3, 2005 anatarajiwa kuolewa hivi karibuni ambapo vikao vya harusi vimeshaanza.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )