Saturday, December 10, 2011

MIKAO YA MASTAA WA KIBONGO NI AIBU TUPU


Kitendo cha baadhi ya mastaa wa kike Bongo kupiga picha katika mikao inayoacha wazi sehemu zao nyeti, kimeelezwa kuwa ni cha aibu huku wadau wakiwataka kubadilika mara moja ili wawe kioo safi mbele ya jamii.

Wakizungumza na mtandao huu  katika nyakati tofauti baadhi ya watu waliodai kukutana mara kibao na picha za ‘mademu’ hao mtandaoni walieleza kuwa, tabia hiyo ni chafu na inaweza kuwafanya wakatafsiriwa tofauti na walivyo.

Walisema, licha ya kwamba kila mmoja ana uhuru wa kufanya vile anavyojisikia, bado kwa maadili ya kitanzania kupiga picha za aina hiyo ni tatizo.
“Wapo wasanii wengi tu ambao kila wanapopiga picha hupenda kuweka mkao wa nne huku wakiwa wamevaa nguo fupi zisizovuka hata mapaja yao.

“Matokeo yake wanajikuta wakianika sehemu zao nyeti pamoja na ‘makufuli’ yao, kitu ambacho siyo maadili kwa mtoto wa kike wa kitanzania. Wanaofanya hivyo wajue wanapata aibu ambayo wanaweza kuiepuka,”dada mmoja alitonya huku akiomba hifadhi ya jina lake
Naye Ibontoko  alisema kuwa, ulimbukeni walionao baadhi ya warembo hao ndiyo unaowasukuma kufanya hivyo bila kujali kwamba wanajichoresha.

“Wenyewe wanadhani huko ndiyo kwenda na wakati na wengine eti wanatumia njia hiyo ‘kujipromoti’, jamani zipo njia nyingi za kutengeneza jina bila kukaa uchi kama hivi, tuache ulimbukeni,”alisema Ibontoko.
Hata hivyo, mara kwa mara baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakitetea staili yao hiyo ya kuvaa nusu uchi na kupozi kihasara huku wakieleza kuwa, wana uhuru wa kuvaa vyovyote wanavyojisikia.

“Nina uhuru wa kuvaa vile ninavyojisikia, wale wasiyofurahia jinsi ninavyovaa watajiju,”aliwahi kukaririwa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu” akisema.
 
Warembo ambao wamekuwa na kasumba ya kupiga picha za sampuli hiyo ni pamoja na mshiriki wa Mashindano ya Miss Tanzania 2005, Jacqueline Patric, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Charamila ‘Ray C’, wasanii wa filamu Elizabeth  Michael, Shamsa Ford, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Salma Jabu ‘Nisha’.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )