Friday, April 6, 2012

MAYASA MRISHO AOLEWA KINYEMELA


TETESI zilizopo mtaani ni kwamba msanii wa filamu, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ameolewa kwa siri na katika kuthibitisha hilo, mwanadada huyo sasa hivi anavaa pete ya uchumba na ya ndoa.

Rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, alichokuwa akijua ni kwamba Maya ana mchumba lakini siku za hivi karibuni ameshangazwa na hatua ya kuolewa kwake kwa siri.

“Mi’ nakwambieni ukweli nina uhakika Maya kaolewa, kama hamuamini mtazameni kidoleni anayo pete ya ndoa na ya uchumba,” kilidai chanzo hicho.

Katika kufuatilia ilibainika kuwa ni kweli msanii huyo anavaa pete hizo na alipoulizwa juu ya taarifa hizo za kuolewa kwa siri alisema:

“Jamani nyie eleweni tu mchumba ninaye lakini bado sijaolewa ila kaeni tayari siku yoyote na mimi nitaitwa Mrs flani."
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )