Friday, May 4, 2012

ODAMA: NAKULA ‘BATA’ KWANZA, NDOA BAADAYE

Mpekuzi blog


MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa kwa sasa hawezi kukurupukia kuolewa hadi atosheke kula starehe ‘bata’ kwa kujinafasi.

Akichonga na paparazi wetu, Odama alisema amefikia hatua ya kusema hivyo kwa kuwa, anajua ndoa inahitaji utulivu kiasi kwamba akiolewa haraka huku akiwa bado ana hamu ya kujiachia anaweza kutibua ndoa.


“Ukiwa ndani ya ndoa utakuwa unabanwabanwa na mwanaume, huwezi kula bata kama unavyoweza kula ukiwa singo kwa hiyo bora nimalizie kabisa nikiingia huko niwe nimetosheka,” alisema Odama.


Akaongeza kuwa, wengi ambao ndoa zao hazidumu wamepapatikia kuolewa ila yeye ataolewa akiwa na miaka 35 na atazaa mtoto mmoja tu.

Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )