Thursday, October 18, 2012

JACK WA CHUZ ANUSURIKA KUPIGWA MAWE ZENJI


WAKATI hali ikiwa bado tete visiwani Zanzibar kutokana na vurungu zinazoendelea, msanii wa filamu kutoka Tanzania Bara Jackline Pantzel ‘Jack wa Chuzi’, amenusurika kuumia katika vurugu hizo wakati akijaribu kukimbia na hata hivyo ameamua kuondoka zenji ili kuepusha balaa ambalo lilitaka kumtokea huko.

Msanii huyo alikuwa visiwani huko kikazi za sanaa, lakini ameshindwa kuendelea na kazi hyo na kuamua kurudi Bara, ili kupisha vurunga hizo na hali itakapokuwa tulivu watarudi tena ili kumaliza kazi waliyokuwa wanafanya.


Akiongea naMwandishi wetu
,Nisha  alisema kuwa vurugu hizo zilimfanya ashindwe hata kula kwani mawe na chupa vilirushwa mfululizo karibu na eneo walipokuwa wamekaa kitu ambacho kimemfanya kuamua kurudi Dar, amedai hata barabara nazo zimefungwa na zimejaa watu eneo lote la mji.

“Yani we acha huku Zanzibar ni kuna vurungu hata hakutamaniki nilikuwa huku kwa ajili ya kazi lakini kutokana hali hii bora nirudi kwanza Dar, nilitaka kurudi jana lakini barabara hazipitiki hivyo leo nimepata usafari wa ndege,”
alisema.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )