Saturday, March 31, 2012

LOWASA AVUNJA UKIMYA......APOKELEWA KAMA MFALME HUKO ARUMERU


HATIMAYE Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amepanda jukwaani kumpigia debe mgombea ubunge wa CCM katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, akiwaambia wananchi wa jimbo hilo kuwa Sioi ni mchapakazi na siyo mtu wa blah blah.

Kupanda jukwaani na kumnadi Sioi kumemaliza mjadala wa kama Mbunge huyo wa Monduli (CCM), angepata fursa hiyo kutokana na kile kilichokuwa kimeelezwa kuwa ni mgawanyiko mkubwa uliopo ndani chama hicho.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa Lowassa alikuwa hatakiwi kupanda jukwaani kumnadi mgombea huyo kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kungekiharibia zaidi chama hicho.

Jana Lowassa alitengua kitendawili hicho saa 7:07 mchana alipowasili kwenye Viwanja vya Kikatiti akiwa na msafara wa magari yasiyopungua 20 yakiongozwa na pikipiki.

Baada ya kufika alipanda jukwaani kwa staili ya kukimbia na baadaye kucheza muziki jukwaani na kushangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo alipohutubia alisema wakazi wa jimbo hilo wanamfahamu kwamba yeye si mtu wa maneno, bali vitendo, hivyo kwa kumchagua Sioi ajenda ya maji itafungwa baada ya mgombea huyo kuapishwa.

Lowassa pia alimmwagia sifa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kuwapatia wakazi wa Kata ya Nduruma, Arumeru eneo la ekari 5,000 akisema ni mchapakazi hodari anayestahili heshima lakini pia Lowassa alikipiga vijembe Chadema akisema kilisababisha maandamano na vurugu katika Jimbo la Arusha Mjini na kuufanya mji huo kutokalika na kuwataka wakazi wa Arumeru wasikichague.

Alisema endapo watamchagua mgombea wa Chadema watakuwa wamefungulia fujo katika jimbo hilo kuanzia Mto Nduruma kuingia wilayani mwao, pia aliipongeza Kamati Kuu ya CCM kwa kupitisha jina la Sioi kuwania ubunge wa jimbo hilo akisema chama hicho kimeonyesha ukomavu wa demokrasia.

Akizungumza katika kampeni hizo, Sioi ambaye alimsifu Lowassa akiwaambia wakazi hao kuwa wanapaswa kuzingatia maneno aliyosema ili wapige hatua kimaendeleo, alisema endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge, atahakikisha anawapa kipaumbele wanawake katika kujiajiri kwa kuwapatia mikopo ya biashara.

Alisema atashirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), katika kufanikisha lengo hilo.
Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema wakazi wa jimbo hilo wanakabiliwa na kero za ardhi, maji na umeme hivyo kumchagua Sioi watakuwa wamechagua dawa ya matatizo yao.

Rais na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akimdai kwa mara ya pili Sioi jana, alitumia muda mrefu kufanya kile alichosema ni kutoa elimu ya uraia kwa vijana waliozaliwa baada ya uhuru akisema wale wanaodai chama hicho hakijafanya lolote ni wehu.

Akionekana kukwepa kujibu mashambulizi kutoka kambi ya upinzani yaliyotokana na hotuba yake kufungua kampeni za CCM wiki chache zilizopita, Mkapa alisema mbele ya CCM vyama vya upinzani ni sawa na vifaranga na chama hicho ni nambari moja.

Akihutubia mkutano uliofanyikia katika Kijiji cha Patandi Tengeru, Mkapa alisema: “Baada ya kuzindua kampeni za CCM yamesemwa maneno mengi dhidi yangu, chama changu na mgombea wetu lakini huu si wakati wangu wa kuyajibu.”
Read More

Msama Promotion yakana kuipa BASATA sh. mil.6

KAMPUNI ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka, imekanusha kulipa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), sh. milioni 6, kama ada a wasanii wanaoingia nchini kufanya maonesho mbalimbali.

Habari hizo zilizoandika na gazeti moja litokalo kila siku (jina tunalo), siyo za ukweli, hivyo ameliomba msamaha baraza hilo kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kuwa, kampuni yake haijatoa fedha hizo zinazodaiwa ni ada ya wasanii wanaokuja nchini kushiriki tamasha hilo.

Msama alisema katika tamasha lililofanyika mwaka jana mgeni rasmi akiwa Rais Jakaya Kikwete, waliomba kupunguziwa gharama za ada hiyo, jambo lililofanyiwa kazi na BASATA.

"Mwaka jana tuliomba kwa Rais Kikwete, atusaidie kupunguza gharama za ada za kuwaleta wasanii, ombi letu lilikubaliwa na likafanyiwa kazi, hivyo hatujapeleka fedha hizo BASATA kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku (jina tunalo)," alisema.

Msama alisema baada ya serikali kupitia baraza hilo kufuatilia kwa makini kazi za kampuni hiyo na kubaini mchango mkubwa wanaotoa kwa vikundi mbalimbali, waliamua kufanyia kazi maombi yote.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa, BASATA lilifuatilia na kushuhudia kampuni hiyo kupitia tamasha la Pasaka wakitoa misaada mbalimbali zikiwemo baiskeli kwa walemavu, mitaji kwa wajane na kuwasomesha watoto yatima.

Tamasha la Pasaka mwaka huu limepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam likiwashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya nchi.
 
Waimbaji kutoka nje ya nchi ni Rebecca Malope kutoka Afrika Kusini, Maryanne Tutuma, Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa wote kutoka Kenya. Kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ni Faraja Ntaboba na Ephraim Seleketi kutoka Zambia.

Msama ameliomba msamaha baraza hilo kwa usumbufu uliojitokeza baada ya habari hiyo kuchapwa katika gazeti hilo, huku akisisitiza kuwa, suala hilo si la kweli.

Msama alisema baada ya maombi yao kusikilizwa na kufanyiwa kazi, serikali kupitia BASATA lilipunguza ada za wasanii kutoka nje na kuwataka kulipa ada ya pamoja ambayo imepunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Read More

Askari polisi wahitimu mafunzo leo chuo cha polisi moshi

 Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani Mh. Mbaraka Abdulwakil, akitoa zawadi kwa mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Polisi mjini Mochi leo. Kulia  ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema,

Gwaride likipita mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa haraka likitoa heshma
Read More

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA OFISI ZA TAWI LA CCM MWANAKWEREKWE B, MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf, wakati alipofika mkoa huo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja. Hapa ilikuwa ni baada ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012
Read More

RIHANNA APEWA MAKAVU.....

INGAWA mwanamuziki Rihanna anaaminika kuwa mwenye mafanikio na mwenye kujituma jukwaani, wapo ambao wanaamini kuwa mwanamuziki huyo hastahili sifa hizo kwa kuwa muziki wake haukidhi viwango.

Mwanamuziki Gene Simmons amesema wazi katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Rihanna ni mmoja kati ya wanamuziki wanaohitaji mafunzo ya kuburudisha na kuimba kwa kuwa bado mchanga katika tasnia hiyo.

"Tumechoka kuwaona wanamuziki wakipanda majukwaani na wacheza shoo huku nyuma yao CD ikiwasaidia kuimba, wakati huo umepitwa," alisema Simmons.

Aliongeza kuwa wasanii wote wakali wanapaswa kupiga muziki wao moja kwa moja na si kutumia CD kama mastaa wengi wanavyofanya duniani, akiwemo Rihanna.

Simmons anasema kuliko aende kwenye shoo ya Rihanna ni bora aangalie kipindi cha American Idol kwa kuwa wanaimba kwa kutumia vyombo moja kwa moja.
Read More

AIBU: WEMA SEPETU AUMBUKA BAADA YA DIAMOND KUKATAA KUPOKEA HELA YAKE JANA USIKU KATIKA SHOW YA DIAMOND'S ARE FOREVER.......

 Huyu ni Diamond akiwa na mama yeke mzazi pamoja na mrembo wake
 Wema sepetu akiwa ukumbini hapo
 Huyu ni Jokate akiwa na rafiki yake
 Diamond aki perform live.....
 Wema Sepetu alienda kumtunza Diamond....Matokeo yake 
 akaishia kuabika baada ya Diamond kuzikataa pesa hizo. 
 Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo 
 zoezi lake halikufanikiwa.

  ...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
  ...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
Uvumilivu ulimshinda Wema sepetu akaanza kulia...pole dadangu...!

Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa 

Cheki hii video inayoonyesha mambo yalivyokuwa
Ni Noma!!! Full kumchunia!
Read More

MASTAA WA MOVIE ZA KIBONGO WAFANYA "UZINZI" KAMBINI


MASTAA waliopiga kambi kwenye hoteli moja  iliyopo Makongo Juu, Dar es Salaam wakirekodi filamu ya Tatakoa, wamenaswa usiku wakiwa wamelala kitanda kimoja jinsi tofauti, kitendo kilichotafsiriwa na watu kuwa ni kichocheo cha uzinzi kwa takribani asilimia 100

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, mastaa hao walinaswa na kamera saa 6:36 usiku wakiwa kwenye chumba kimoja chenye vitanda viwili, lakini kimoja kikiwa kimelaliwa na wasanii wenye jinsia tofauti bila kujali ni mke, mchumba wa mtu na kondom huonekana zikizagaa ovyo wakati wa asubuhi.
 
Msanii mmoja wa kiume ambaye  jina lake halikupatikana mara moja inasemekana huonekana kwenye Tamthiliya ya Red Apple, wa kike ni Zerishi aliyewahi kutamba na Kundi la Chemchemi Arts Promotion ‘Kidedea’.

Kitanda cha pili, walilala Dora Redson ‘Kadadaa’ (msanii wa zamani wa Kaole Sanaa Group) na staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.

 
Baada ya kuiweka kibindoni picha hiyo,mpekuzi wetu alimuuliza Kadadaa uhalali wa kupiga kambi huku wasanii wenye jinsi tofauti wakitumia kitanda kimoja ambapo alifunguka kwa kusema:

“Mh! Unajua wakati mwingine watu wanakuwa wamechoka tu, wanapumzika, lakini inategemea uhuru wa mtu. Mimi kambini huwa nalala na wanawake wenzangu.” 

Baada ya kuzungumza na Kadadaa, mpekuzi wetu  alimwendea hewani Nisha ambaye kwa upande wake alisema:

“Aaaa, hapo tulikuwa kwenye shooting, wala hakuna tatizo kabisa.”

Msanii Zurishi yeye hakupatikana kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia ishu hiyo.


Uchunguzi zaidi i umebaini kuwa, vitendo vinavyofanywa na wasanii wanapokuwa kambini havitazamiki licha ya kwamba, baadhi yao wana familia.

Nyota mmoja  alisema kuwa, mara nyingi mastaa wanaporekodi sinema, hugeuza kambi kuwa kilinge cha mambo yasiyofaa.

“Kama ni uchafu sisi wasanii nafasi yetu ni kambini. Kule hapajalishi umeolewa, umeoa. Hata yule ambaye akiwa nyumbani familia inambana, basi humalizia machungu yake kambini.

“Wapo wasanii ambao wakati wa kuwekodi, wapenzi wao huja kambini na wao huwa wapole lakini wakiondoka usiku, kazi huanza hapo, pombe kwa sana, mapenzi usiseme, mpaka unajiuliza hivi kweli huyu kaolewa au ameshaachika ?” Alisema staa huyo wa kike.


Mpekuzi pia lilizungumza na bosi wa Kampuni ya Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ na kumuuliza kama kambini kuna tabia hizo.

“Ah! Si kambini tu, hata mitaani zipo. Kikubwa watu wanaangalia zaidi kambini kwa sababu jamii moja inakusanyika kwa wakati mmoja, unataka kuniambia mtaani, wake za watu au waume za watu hawatoki nje ya ndoa zao?

“Sisi tunachukua wasanii kwa makubaliano ya kushiriki filamu tu, tabia binafsi ni vigumu sana kuzidhibiti kwa sababu ni watu wazima na hazipo kwenye mikataba,” alisema Chuz.
Read More

WAREMBO WAFANYA MAMBO YA AIBU UKUMBINI


Baadhi ya mastaa waliotimba kwenye pati ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Kimwana Manywele 2006, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’ wanadaiwa kugeuza ukumbi kuwa uwanja wa ufuska kufuatia matukio machafu waliyoyafanya


Tukio hilo lililoshuhudiwa na mpekuzi wetu lilichukua nafasi usiku wa kuamkia Alhamisi ya Machi 29, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sumit Kinondoni Mkwajuni jijini Dar ambapo mtangazaji huyo wa zamani wa C2C alikuwa akitimiza miaka kadhaa .


Awali, shughuli hiyo ilianza vizuri kwa ‘mtoto aliyezaliwa’ (Aunt Lulu) kuingia ukumbini akiwa amevalia kiheshima ambapo shampeni ilifunguliwa na wageni kula na kunywa huku wakimpongeza staa huyo.

Wakati pati hiyo inakaribia ukingoni, ghafla Miss Mara na Miss Tanzania 2001, Rashida Wanjara aliyeingia ukumbini hapo dakika kadhaa zilizopita alimmwagia Aunt Lulu ‘minoti’ ya elfu kumi kumi iliyokadiriwa kuwa zaidi Sh. laki 3.

Wakati watu wakiendelea kutandika ulabu, ghafla vijana watano wanaodaiwa kuwa ni mashoga walianza kushindana kukata nyonga ukumbini humo, hali iliyofanya kila mtu kubaki kuwatazama wao.


Mastaa waliofika ukumbini humo wakiongozwa na Isabella Mpanda, Rashida Wanjara, Aunt Lulu na wengine wengi walitia chumvi sherehe hiyo baada ya kucheza kihasara na kuacha maungo nyeti hadharani.

Pia baadhi ya warembo wanaojiita wadada wa mjini walipigwa chabo wakidendeka laivu wenyewe kwa wenyewe hivyo kusababisha pati hiyo kukumbushia enzi za Sodoma na Gomora kufuatia matukio hayo machafu.

Aunt Lulu ambaye siku hiyo alionekana mpole alidai kuwa, anajisikia vibaya kila siku kuandikwa akiwa na mavazi ya hasarahasara hivyo kuamua kubadilika kwa kutoka kitofauti siku hiyo.
Read More

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA TUZO ZA (AJET) USIKU WA LEO DIAMOND JUBILEE

 Rais Jakaya Kikwete akiongea na Fili Karashani Mwandishi mkongwe naambaye ameshinda  tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari Nchini Tanzania (MCT) na washirika wake, hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu, katika picha kushoto ni Mwandishi wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Nevil Meena cheti cha ushindi wa jumla kwa katika tuzo hizo mara baada ya kutangazwa rasmi.
 Kikundi cha Ngoma za asili cha Simba Thietre kikitumbuiza katika tuzo hizo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandhishi wa habari wa Mlimani Radio Tuma Dandi mshindi wa habari za watu wenye ulemavu- Redio
 Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda akikabidhi tuzo kwa Abdallah Majura Mkurugenzi wa Radio Sports FM ya Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws akimkabidhi cheti na zawadi yake Nevil Meena kutoka gazeti la Mwananchi.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Executive Solution Agrey Maleale akimkabidhi zawadi yake Khamis Hamad kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo.
 Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi walipokutana katika hafla hiyo
Read More

Friday, March 30, 2012

PENZI LA SHAROPOVA NA J4 SIYO SIRI TENA


Baada ya kujificha sana hatimaye uhusiano wa kimapenzi wa wasanii wawili wanaopiga mzigo kwenye Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Asha Saidi ‘Sharapova’ na Jumanne  Saidi ‘J4’, siyo siri tena.

Hilo lilibainika juzikati maeneo ya Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya wawili hao kunaswa wakiwa wamegandana kimahaba na baada ya kubanwa sana walikiri kuwa ni wapenzi.

“Unajua uhusiano wetu ulikuwa haujulikani kwa watu kwa sababu maalum lakini kwa sasa hatuna sababu ya kuficha, huyu ni mpenzi wangu na lengo ni kuoana,” alisema Sharapova.

Kwa upande wa J4, alisema: Hatuna sababu ya kuendelea kujificha, huyu ni wangu na watu hasa wanaume wakware wanatakiwa kujua ili wasimsogelee.
Read More

PICHA ZA MIMBA YA WASTARA JUMA ZAVUJA.....


Picha za kipindi cha ujauzito wa msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma zimevuja baada ya kuzificha kwa muda mrefu.

Picha hizo ambazo zinamuonesha Wastara akiwa ameliacha tumbo lake wazi siku chache kabla ya kujifungua na nyingine akiwa kwenye mapozi ya ‘kimisi’ zilinaswa na mpekuzi wetu kupitia kwa rafiki yake wa karibu.

Baada ya kuziweka kibindoni, Mpekuzi wetu alimwendea hewani msanii huyo na kumuuliza sababu za kujificha akiwa mjamzito ambapo alisema ilikuwa ni makubaliano yake na mumewe kutokana na matatizo yaliyokuwa yakiwakabili.


“Kuna mambo yalijitokeza ndiyo maana ikawa hivyo lakini sasa kama mmezipata sioni kama ni tatizo Watanzania wakaniona nilivyokuwa wakati nilipokuwa mjamzito,” alisema Wastara.
Read More

ZAMARAD AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUJIFUNGUA SALAMA...


Mtangazaji wa Kipindi cha TAKE ONE cha Clouds TV, Zamaradi Mketema juzikati alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aga Khan na kumshukuru Mungu kwa kuutua mzigo huo salama.

Akichonga na mpekuzi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Zamaradi alisema kipindi chote cha ujauzito wake kuna waliodhani angejifungua kwa operesheni lakini Mungu amekuwa upande wake.

“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kuniwezesha kujifungua salama kwa njia ya kawaida. Nafurahi kumpata mtoto huyu wa kiume na huu ni mwanzo wa maisha mapya,” alisema Zamaradi.

Mtangazaji huyo amejifungua zikiwa zimebaki siku chache kwa wasanii wa filamu Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na  Shamsa Ford nao wajifungue.
Read More

Thursday, March 29, 2012

GAZETI LA "RAIA MWEMA" LAPEWA ONYO NA SERIKALI

Read More

CAG Akabidhi Ripoti Kwa Rais

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akikabidhi ripoti yake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni naibu mdhibiti n Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Atanas Tarimo(picha na Freddy Maro
Read More

WASANII MAARUFU BONGO WADAIWA KUJIUZA NA KUPIGA PICHA CHAFU WAKIWA NCHINI KENYA


Wasanii wanaoendesha maisha yao kwa ‘kuuza nyago’ kwenye filamu za Kibongo, Kelvina John na Edna Gabriel, wanadaiwa kufanya ufuska wakiwa nchini Kenya ikiwa ni pamoja na kujiuza na kupiga picha chafu.

Chanzo chetu makini  ambacho kipo nchini humo hivi karibuni kilitonya kuwa, wasanii hao walifanya uchafu huo wakiwa jijini Nairobi ambako walikwenda kwa shughuli ambayo haikufahamika.

“Kwa kweli hawa mademu wamepinda, yaani wamediriki kupiga picha chafu wakiwa katika hoteli moja hapa Nairobi na walikuwa wakijichanganya katika klabu ambazo baadhi ya wanawake hucheza uchi na kujiuza, mimi kwa kuwa nawajua nilipowaona nilishangaa sana,” kilidai chanzo hicho.

Kikaongeza kuwa, walivyoonekana wasanii hao ni kama walikwenda kwenye jiji hilo kwa lengo la kufanya ufuska wakijua huko hakuna atakayewajua.

Katika kuweka mambo sawa, mpekuzi wetu alimtafuta mmoja wa wasanii hao, Kelvina kuzungumzia skendo hiyo na alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:

 “Sisi tulipiga picha zetu wenyewe kwa matakwa yetu sijui kwa nini mtu alizichukua na kuwaletea? Na hilo suala la kuingia kwenye klabu za wacheza uchi tuliingia tu kama moja ya kumbi za starehe lakini siyo kwamba tulienda kucheza au kujiuza kama mlivyoambiwa.”
Read More

HALI YA VENGU INAENDELEA VIZURI.....HIVI SASA ANAWEZA KUSIMAMA NA KUKAA MWENYEWE


MUNGU ni mkubwa! Hatimaye dua za Watanzania zimesikika kwa staa wa Kundi la Orijino Komedi aliyepo Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu, Joseph Shamba ‘Vengu’ (pichani) ambaye ameinuka na kukaa mwenyewe kitandani.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambaye ni mtu wake wa karibu, mbali na hatua hiyo, pia nyota huyo ameanzishiwa mazoezi ya kuongea baada ya kitambo kirefu kutomudu kuzungumza.

Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa, jitihada kubwa zilifanywa na madaktari wa Hospitali ya Appolo ili kuhakikisha kuwa Vengu anarudi katika hali yake ya kawaida.

“Dalili zimeanza kuonekana, hivi sasa Vengu yuko katika hali nzuri, anaweza kuinuka na kukaa kitandani ila bado anapewa mazoezi ya kuongea,” kimesema chanzo hicho.

Habari zaidi zilisema kuwa kinachomfanya Vengu kushindwa kuzungumza vizuri ni kupoteza kumbukumbu kwa muda mrefu na kufanya mdomo wake kuwa mzito.

“Jumatatu (Machi 27, mwaka huu) madaktari walianza kumfanyisha mazoezi ili aweze kuzungumza vizuri, ingawaje haijulikani zoezi hilo litachukua muda gani,” kilisema chanzo hicho na kudai kuwa kama Vengu angeachwa Tanzania, asingefikia katika hatua aliyonayo sasa.

Mbali na kufanyishwa zoezi hilo la kuzungumza, pia Vengu ameanza kufanyishwa mazoezi ya viungo ili kumfanya aweze kutembea mwenyewe.

“Madaktari wameonekana kufurahishwa na hatua hiyo na wanamfanyisha mazoezi ya viungo na kumzoesha kuongea kama unavyojua ana siku nyingi hajazungumza,” kilisema.

Baada ya kupata taarifa hizo, mpekuzi wetu alimtafuta ndugu wa karibu wa Vengu ambaye anaishi jijini Dar lakini hakuweza kupatikana kuzungumzia hali ya staa huyo.

Hata hivyo, Mpekuzi wetu alifanikiwa kumpata mchumba wa Vengu ambaye ni Miss Kinondoni 2011/12, Stella Mbuge na kumuuliza kama ana taarifa zozote kuhusiana na mgonjwa huyo, naye alisema ameambiwa na kaka wa Vengu kuwa sasa jamaa yake yuko katika hatua ya kufanyishwa mazoezi ya kuongea.

“Kaka yake amefurahishwa na hali ya Vengu na amenihakikishia kwamba anaendelea vizuri, kwa sasa anaweza kuinuka na kukaa mwenyewe ila wanamfanyia mazoezi aweze kuongea tena,” alisema kwa kifupi Stella.

Vengu alianza kuumwa mwaka 2009 ambapo Agosti, mwaka jana alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi akisumbuliwa na ugonjwa unaoshambulia sehemu ya kichwa, hasa ubongo.
Read More

"NIMECHOKA KUCHAFULIWA MBELE YA JAMII"...ROSE NDAUKA

MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Rose Ndauka Aisha, ameibuka na kusema kuwa watu wanajaribu kumharibia na kumtangazia tabia ambayo si yake, jambo ambalo linamchafua mbele ya jamii.

Inasemekana tangu mrembo huyo mwenye jina katika tasnia ya filamu aanze kuishi kama mke amekumbwa na kashfa nyingi huku akiambiwa kuwa sasa anatumia kilevi.

Hali hiyo imewafanya baadhi ya wanajamii kuhisi huenda mwanadada huyo kakumbwa na msongo wa mawazo.

Mpekuzi wetu alimtafuta Rose na kuzungumza naye kuhusu shutuma zinazomkabili kama chanzo ni uhusiano huo mpya au la.

Ni kweli, hata mimi kuna baadhi ya maneno nayasikia kuhusu uhusiano wetu na mwezangu, lakini si ya kweli, na ikumbukwe kuwa sisi bado ni wapenzi, kwani hatujafunga ndoa.
"Kwa hiyo hata mtu akiniuliza maisha ya ndoa siwezi kumjibu kwa sababu bado sijaishi, kwa sasa tupo katika uchumba na maisha yetu yako poa", anasema Rose.
Pia amesema kuwa uhusiano wake na mpenzi wake si tatizo kwani hazuiwi kufanya lolote linalohusu filamu, lakini anapopata kazi ni vema kumjulisha mwenzi wake kwa sababu hana kipingamizi kwani huko ndiko alikomuona.

Anasema yeye ana uhuru wa kufanya kazi wakati wowote ilimradi iwe na maslahi kwake, huku akiongeza kuwa uhusiano wake na mpenzi wake uko shwari.
Read More

STEVEN NYERERE AMPA MAKAVU JACOB STEVEN "JB"

 
MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood, Steven Mangere Nyerere, katika hali ya masihara alitumia muda huo kumpiga dongo msanii mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Jacob Stephen JB kwa kueleza kuwa JB pamoja na kumiliki kampuni na sasa ni kinara wa mauzo, lakini kampuni yake haina hata ofisi kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, tofauti na nyota wenzake kama Ray, Kanumba na Mtitu na Richie.

Steve Nyerere, msanii mwenye staili yake ya kipekee katika kujitafutia fedha ambaye awapo kazini yupo tayari kufanya jambo lolote ili apate pesa, alimshushia madongo hayo wakati wa sherehe za Bongo Movie Club kutimiza mwaka mmoja wa kuundwa kwake. Kundi hilo linaundwa na wasanii nyota na chipukizi.

"JB bonge la mume, bonge la bwana, tumbo kubwa lakini pamoja na kumiliki tumbo ndiye msanii asiyekuwa na ofisi, huyu anampenda na kumheshimu mkewe, lakini jamaa hana ofisi kwa ajili kampuni yake", Steve alisema hayo huku akicheka.

Msanii huyo alizidi kusisitiza kuwa alikuwa akitania katika kuwataja wasanii na kuoanisha na matukio yao ya kweli huku akisema; "Leo nawatuza wasanii kulingana na matukio yao, leo nawapa tuzo zao kwa matukio yao, si unaona kama JB hana ofisi, msanii mkubwa huyo"
Read More

SPONSORSHIP YA MASOMO KWA MWAKA 2012/2013 KATIKA CHUO KIKUU CHA MUIS - AUSTRALIA....WAHI MAPEMA


JINA LA SCHOLARSHIP: Macquarie University International Scholarship

UTANGULIZI:
Macquarie University International Scholarship (MUIS) ni scholarship kwa ajili ya wanafunzi wa  shahada ya kwanza(undergraduate) na shahada ya pili kwa mwaka wa masomo wa 2012/2013

 NI MASOMO GANI YANAYOKUBALIKA?

Hizi scholarship za MUIS zinatolewa kwa masomo yote ya chuo kikuu cha MUIS isipokuwa : Business Administration (MBA), Management, Applied Finance, Advanced Surgery, and Surgery

TAARIFA ZAIDI KUHUSU HIZI SCHOLARSHIP.
Chuo kikuu cha MUIS kinatoa scholarship kwa raia wa nchi zote isipokuwa Australia na New zealand.
Ufadhili huu unajumuisha malipo yote ya Ada kuanzia mwaka huu wa masomo wa 2012/2013

AINA YA SCHOLARSHIP: FULL SCHOLARSHIPNI SIFA GANI UNATAKIWA UWE NAZO?

 • Usiwe raia wa Australia au New zealand.
 • Uwe umetimiza vigezo vya course husika na vigezo vya lugha ya kiingereza.
 • Uwe na GPA ya 3.7 kati ya 4.0 au 2.7 kati ya 5.0 kwa wale wanaotarajia kuchukua masters.Uwe na ATAR ya point 92 kati ya 100 kwa wale wanaotegemea kuanza degree zao
Huwezi kupata schorship endapo:
 • Wewe ni raia wa Australia au New Zealand.
 • Tayari ni mwanafunzi wa chuo hicho katika course yoyote.
 • Umewahi somea kitu hicho hicho katika chuo hicho miaka ya nyuma.
 • Tayari una udhamini/sponsor mwingine.
JE NI SCHOLARSHIP ZA WATU WANGAPI?  Ni  watu kadhaa tu,wahi mapema
Utafaidikaje?
Chuo hicho hutoa udhamini wa malipo ya ada kwa kipindi chote cha masomo.

Angalizo:
wao hawatoi udhamini wowote kwenye mambo yafuatayo living allowance, gharama za visa , Overseas Student Health Cover (OSHC), airfares na accommodation.

 WATAKUDHAMINI KWA MUDA GANI?

Kwa kipindi chote cha masomo.

NI NCHI ZIPI TOKA AFRIKA NDO ZINATAKIWA?
>>>ZOTE

Utapelekwa nchi gani?: Macquarie University, Australia

Maombi yatafungwa lini?
Semester 2, 2012             30 April 2012
Semester 1, 2013             31 October 2012
Semester 2, 2013             30 April 2013

Je,udhamini wao ni wa  kila siku? NDIYO

Jinsi ya kuomba hizo schorship
Kamba maombi yako yatakubaliwa,basi chuo hicho kitakutumia namba ya usajili ili ikusaidie kuomba ufadhili/scholarship za MUIS .
 • Ili kujaza hizo form za scholarship,basi bofya hapa << online MUIS application form.>>
 • Usisahau kuchagua aina ya scholarship kati ya hizi pindi utakapokuwa unajaza:
  • MUIS Undergraduate
  • MUIS Postgraduate
Ntapataje maelekezo zaidi?
Kama unahitaji maelekezo zaidi,basi bofya hapa << Scholarship Webpage>>

Mfadhiri ni nani
Chuo kikuu cha Macquarie - Australia

Maelekezo muhimu:
1.Uwe na referee/wadhamini wawili.
2.Andika 'page' moja ukielezea kwa nini umeamua kuomba hiyo scholarship
3.Maelezo yote yakusanywe katika muundo wa PDF au Ms word na isizidi kb 256.
4.Form ambayo haijatimiza mashart haitashugulikiwa.

Kama umeipenda ripoti hii, basi usisahau kuninunulia japo vocha kwa namba 0768 837 613.na kama una maoni,basi niandike comment  hapo chini
Read More

WEMA SEPETU AITWA KWA "SANGOMA"


Wema  Sepetu ambaye kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akisakamwa na matatizo ya kimapenzi ameitwa kwa mganga wa tiba za jadi,anayejulikana kama Sharif Abdallah kwa ajili ya kupewa msaada wa tatizo lake hilo.

"Najua kinacho msumbua,mwambieni aje ili niweze kumsaidia.Wengi wenye matatizo kama hayo wamefanikiwa" Alijinadi mganga huyo mbele ya mpekuzi wetu
Read More

SHILOLE AANZISHA KUNDI LA KUCHEZA UCHI


Wakati baraza la sanaa taifa (BASATA) likitangaza kuimarisha maadili ya sanaa za maonesho hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuyanyooshea kidole baadhi ya makundi yanayo anzishwa kiholela na kufanya maonesho ya nusu uchi,msanii wa filam ambaye hivi sasa anang'aa kupitia fani ya muziki Zuwena Mohamed "Shilole"  ameanzisha kundi lake la unenguaji la nusu uchi

Kundi hilo ambalo hulitumia kunengua katika kumbi mbali mbali za starehe anapofanya maonesho hivi sasa  limekuwa gumzo kubwa kutokana na staili za kumwaga radhi jukwaani kama ilivyo kwa makundi ya khanga moja,laki si pesa, kitu tigo na wela wela

Tayari Shilole ameanza kula shavu la kupiga maonesho jijini Dar huku waneguaji wake watatu wa kike wakionesha manjonjo ya kuonesha nguo zao za ndani.

Hali hiyo imemfanya pia msanii huyo kuanza tabia ya kujipekua nguo akiwa jukwaani ili kuendana na wanenguaji wake kitendo kinacho tafsiriwa kuwa kitamweka pabaya
Read More

RAY C ANASA KWA MKONGO


Mwanamziki mahiri wa bongo fleva,Rehema Yusuf Chamilla "Ray C" ambaye kwa sasa makazi yake ameyahamishia huko nchini Kenya anakofanyia kazi zake za muziki ameupasha mtandao huu kuwa,kwa sasa shughuli zake amezitia chini ya uongozi wa raia mmoja wa Congo.

Akiongea nasi mwishoni mwa wiki jana, mwanadada huyo anayesifika kwa kunengua jukwaani amesema kuwa mkongo huyo aliyemtaja kwa jina la Paul Limumba ndiye meneja wake kwa sasa,hivyo yeyote anayetaka kufanya naye kazi awasiliane naye.

"Tangu nianzishe bendi yangu inayokwenda kwa jina la Ray C band ,nimekuwa na mambo mengi ya kufanya kama msanii,hivyo nikafikia uamuzi wa kugawa majukumu mengine ya kiuongozi kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ya uongozi kwa makini",alisema

Aliongeza kuwa "Meneja wangu ni mbunifu sana.watu wanaweza kuwasiliana nami kisha nikawaunganisha nae maana kafanikiwa kuifanya band yangu itambulike kwa haraka nchini Kenya na Rwanda"
Read More

Wednesday, March 28, 2012

SINTAH ATAFUTA MWANAUME WA KUMZALISHA


 STAA wa Filamu na Maigizo Bongo, ambaye kwa sasa anachapa mzingo Kwenye kipindi cha Hatua Tatu kinachorushwa hewani kupitia 100.5 Times FM, Sintah Manongi 'Sintah JLO Africa', juzikati alifyatuka kwa kusema kuwa anahitaji bwana wa kuzaa naye maana amezidi kusemwa kila  kona na ndugu na marafiki zake wa karibu.
 
  Akiongea na mpekuzi wetu, Machi 27 mwaka huu Sintah alisema kuwa, amefikia kusema hivyo kwa kua tayari umefikia wakati wake wa kuitwa mama maana siku zinazidi kwenda mbele na  akisema asubiri ndoa ndiyo azae bado itazidi kumchukua muda mrefu kumpata atakayeendana naye kitabia kama ndoto zake zilivyo siku zote.

"Niko Smakini sana  na jambo  hili na wala sitanii tena maana sasa nimezidi kukoseshwa raha na marafiki zangu kila mmoja ukiongea naye habari zinazohusiana na mtoto basi utasikia ananisema tena wakati huo anakuwa hatanii hata kidogo, sasa kuepusha maneno nitazaa pale tu nitakapopata mwanaume wa kuzaa naye", alisema Sintah a.k.a JLO Africa
Read More

RAIS KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA MIKAKATI YA KUONDOA UMASKINI LEO JIJINI DAR


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  akitoa mada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili ya REPOA. Wengine toka shoto  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.
Profesa Do Duc Dinh toka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  kwa mada nzuri. Kati yao ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.
RaisDkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa kwa hotuba nzuri ya ufunguzi na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa .Samuel Wangwe .
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.
Read More