Thursday, August 22, 2013

TUNDAMAN AFANIKIWA KUWATOROKA POLISI AKIWA NUSU UCHI....KISA NI DENI LA LAKI NANE


Msanii Tundaman amejikuta akiambulia aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani akiwakwepa askari polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa lengo la kumkamata....

Chanzo cha Tunda man kusakwa na polisi ni deni la sh. laki nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mwanadada mmoja ( jina kapuni).... 

Taarifa zinadai kwamba, baada ya kupewa hela hiyo, Tunda man aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa mrembo huyo. Kila akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi ya nguoni..... 

Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo aliamua kulifikisha swala lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa mikononi mwa polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni lake kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013 

Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza kulipa kiasi chochote na wala hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyomfanya mwanadada huyo arudi kuripoti polisi.... 

Polisi walianza jitihada za kumsaka ambapo leo majira ya saa nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana ) kwa lengo la kumkamata..... 

Bahati nzuri au mbaya, Tundaman alifanikiwa kuwatoroka polisi akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa mashuhuda) na kutokomea kusikojulikana...

Ifuatayo  ni  HATI  YA  MAKUBALIANO  yao  ambayo  mpekuzi  wetu  amefanikiwa  kuipata....

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )