Saturday, September 21, 2013

Picha za serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa karume mjini musoma mkoani mara usiku wa leo Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.

 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara

 Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma

 Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.

 Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

 Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma usiku huu

Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta

Makamuzi yakiendelea jukwaani

 Sehemu ya umati wa watu.

 Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee akiimba jukwaani wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013  ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.

 Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa  kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.

Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.

 Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume

 Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume

 Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya watazamaji waliojitokeza  kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.

 Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani


 Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 

 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.

 Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )