Saturday, September 14, 2013

SHEMEJI yangu ananitaka kimapenzi....Naombeni ushauri wenu

 
Nina rafiki yangu ambaye ni kama ndugu,tumetoka mbali sana na sasa ni kama mtu na kaka yake.Jamaa yangu huyu(hajaoa) alikuwa na dem flani  lakini walishindwana kwa matatizo yao binafsi wakawa wameachana kama mwaka mmoja uliopita. 

Kwa kuwa nilikuwa nishatambulishwa kwa shemej yangu huyo basi hata baada ya kuachana na jamaa yangu tukawa tunasalimiana,iko siku ananipigia na mimi kuna siku nampigia kumsalim. Tunaitana shemeji.


Kuna kipindi shemej yangu huyo alikuwa na shida ya hela.Kwa kuwa hakuweza kumwambia ex wake basi aliniambia mimi lakini nilimtonya ex kuwa mwenzake alikuwa na shida...

Jamaa hakutaka kumsaidia kabisa ex wake,nikachukua jukumu la kumsaidia huyo shem wangu.Basi mawasiliano yakawa yapo kama kawaida kwa shem wangu huyo.

 Kuna siku shem aliniuliza kama mke wangu yupo nyumbani,nikamwambia alikuwepo lakini keshaondoka kurudi kazini kwake mkoani  na ana kama miezi  miwili sasa.  
 
Basi shem akawa akinipigia simu hadi usiku  wa  manane   kunisalimia na kunitakia usiku mwema. Mwisho wa siku shem akaniuliza nawezaje kuishi muda wote huo wakati   mke wangu hayupo? 

Nikamjibu navumilia tu, akaniambia kweli huo ni muda mrefu ila endapo nitakuwa na shida yoyote yuko tayari kunisaidia...

"Nakuonea huruma shem wangu, muda huo ni mwingi sana kwa mwanaume,endapo utahitaji kampani yangu niko tayar kukusaidia kwa lolote wakati mkeo  hayupo,kwani hata huyo jamaa yako mi siko nae tena". Hii  ni  message  aliyonitumia
 
Niliingiwa na uoga sana lakini nikajikaza na kumwambia jamaa yangu kuwa ex wake kanipa ofa ya kapani yake na niitumie nitakavyo.Jamaa akanijibu kuwa yeye alishamalizana nae na hana sababu tena ya kurudiana nae, kama nina uwezo wa kutumia ofa hiyo basi niendelee nayo. 


Wadau hiyo ndo hali niliyonayo kwa sasa,naomba mwenye ushauri mzuri   anisaidie


Mdau.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )