Thursday, March 24, 2016

Rais Magufuli Atoa Zawadi Ya Pasaka Ya Milion 9 Kwa Watoto Yatima na Wazee Wasio Jiweza


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa zawadi mbalimbali zenye  thamani ya shilingi milioni tisa laki tatu na elfu sabini kwa vituo 24 vya kulelea watoto yatima na wazee wasiojiweza nchini kwa lengo la kuungana nao katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka.

Msaada huo uliotolewa na Rais ni pamoja na Mchele, Mbuzi na mafuta ya kupikia ambao utakwenda kwenye vituo 6 vya watoto yatima vilivyoko jijini jijini Dar es salaa, na vituo viwili vya Zanzibar, Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Kagera na Morogoro na kituo kimoja kwa mikoa ya Tanga, Ruvuma, Shinyanga, Mtwara na Mara.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais kwa wafanyakazi wa vituo hivyo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi amesema kuwa msaada huo uliotolewa na Rais Magufuli ni moja ya utaratibu wa kawaida wa Marais tangu awamu nne zilizopita kuwapatia zawadi makundi maalum vyakula ili kuwawewezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu mbalimbali kama wananchi wengine wa kawaida katika jamii.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )