Monday, March 21, 2016

TPDC Yatoa Ufafanuzi Juu Ya Ugunduzi Wa Gesi Asilia Bonde La Ruvu Mkoa Wa Pwani


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu shakani”. 
 
Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia trilioni 2.17 una mashaka. 
 
TPDC inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015. Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo: 
 
1. Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”
 
2.   Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima “pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa gesi
 
3.   Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine. 
 
Baada ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo.
 
Taarifa hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF). 
 
Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa. 

Kwa kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa trilioni 2.17. 
 
Mkandarasi atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal program”.
 
Mnamo Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na 65.

Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )