Saturday, April 30, 2016

Abiria Wanusurika Kufa Katika Ajali ya Ndege Mjini Bukoba Leo

Ndege iliyokuwa na abiria wanane na rubani wawili imeacha njia baada ya tairi la kulia kupasuka wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba ikitokea Mwanza.

Tukio hilo limelotokea leo saa 10.32 asubuhi na kusababisha taharuki kubwa kwa wananchi ambao walizunguka uzio wa uwanja wa ndege kushuhudia abiria waliokuwa wakitoka baada ya kunusurika kifo.

Meneja wa Uwanja wa ndege wa Bukoba, Doris Uhagile alisema abiria wote katika ndege hiyo ya kampuni ya Auric wametoka salama na baadaye kampuni hiyo ilituma ndege nyingine kuwachukua waliokuwa wamekwama baada ya ajali hiyo.


Pia meneja huyo alisema awali safari ya ndege hiyo kwenda Bukoba ilikuwa imecheleweshwa kwa muda kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa.


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )