Thursday, April 21, 2016

Bungeni: Mbunge Apendekeza Serikali Ipange Bei Elekezi ya Maziwa


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Gibson Ole Maiseyeki (Chadema) amesema bei ya maziwa nchini ni ndogo kuliko ya maji, hivyo kuitaka Serikali kupanga bei elekezi ya bidhaa hiyo ili kuleta tija kwa wafugaji.

Maiseyeki alisema Tanzania ni nchi ambayo wafugaji huuza maziwa kwa bei ndogo, kuliko nchi nyingine duniani.

 “Ni lini Serikali itakuja na bei elekezi ya maziwa, ili kuipa tija sekta ya wafugaji nchini?” alihoji Maiseyeki.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema bei ya bidhaa mbalimbali zinatokana na nguvu ya soko.

Katika swali la msingi, Maiseyeki alitaka kufahamu jitihada za makusudi za Serikali kuwatafutia wafugaji mbegu bora za mifugo, huku akiwasambazia kwa bei nafuu ili kuondokana na aina ya mifugo ambayo haina tija. 

Ole Nasha alisema Serikali inajitahidi kuhakikisha wafugaji wanapata mbegu bora za mifugo kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwamo uhawilishaji.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )