Thursday, April 28, 2016

Halmashauri ya Rombo Hatarini Kufutwa


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki amesema Halmashauri Wilaya ya Rombo iko hatarini kufutwa kutokana na kushindwa kufikia lengo la Serikali la kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vyake.

Sadiki alisema hayo jana wakati akizungumza na madiwani, wenyeviti wa vijiji na wakuu wa idara wa halmashauri hiyo.

Alisema wilaya hiyo inatumia asilimia 93 ya ruzuku kutoka serikalini hali inayosababisha kuwa hatarini kufutwa kwa kushindwa kukusanya mapato.

Mkuu wa wilaya hiyo, Lembris Kipuyo aliitaka halmashauri hiyo kubuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo iliyojiwekea.

Alisema Serikali imetangaza halmashauri ambazo zitashindwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 ifikapo Juni mwaka huu zitafutwa. 

“Serikali haina lelemama ikifika hiyo tarehe kama mmeshindwa kufikia lengo itafutwa, taarifa nilizonazo mko asilimia 43 hali ambayo ni hatari kwa halmashauri ambayo iko mipakani mwa nchi nyingine,” alisema Sadiki.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )