Wednesday, April 20, 2016

Hiace Yateleza Kwenye kivuko, Yatumbukia bahari Ya Hindi


Jeshi la Zimamoto linaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari aina ya Hiace ambalo limetumbukia bahari ya Hindi leo alfajiri mara baada ya kuteleza kutoka kwenye kivuko kilichokuwa kinaelekea upande wa Kigamboni.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo, Briton Monyo, ajali hiyo imetokea majira ya saa 10 alfajiri na hadi sasa wameweza kuupata mwili dereva wa gari hilo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 29-30.

Monyo anasema gari hilo litakuwa limetitia chini kwa eneo ambalo tukio limetokea lina kina kirefu cha maji, tope jingi na vumbi na huku jeshi likiwa halina vifaa vifaa kama darubini ya majini.

Hata hivyo, ndugu wa mwanamke anayetafutwa wanasema jana walitoka Mbeya kwenye msiba wa ndugu yao na gari walilopanda la magazeti liliwaacha eneo Feri saa 10 alfajiri wakati huo kivuko kilikuwa kimefika ndipo walipoingia na kukutana na Hiace na kukubaliana na dereva kuwafikisha makwao mara baada ya kuvuka ng’ambo ya pili.

Hata hivyo, mwanamke huyo alikuwa amechoka na kuingia ndani ya Hiace  huku ndugu wengine tisa wakakaa sehemu ya abiria ya kivuko.

“Lakini kabla panton halijaanza kuondoka tulishangaa Hiace ikiserereka na kutumbukia” mmoja wa ndugu hao alisema.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )