Wednesday, April 20, 2016

Liyumba Kuagwa leo Jijini Dar es Salaam, Kuzikwa kesho Morogoro


Maziko ya mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba yatafanyika kesho mkoani Morogoro baada ya kukamilika kwa taratibu za kuaga mwili wake leo jijini Dar es Salaam.

Liyumba alifariki dunia juzi saa 10.00 jioni katika Hospitali ya Aga Khan kutokana na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu mpaka dakika ya mwisho. 

Akizungumzia taratibu za mazishi, msemaji wa familia, Moses Liyumba alisema marehemu atazikwa nyumbani kwake Morogoro. 

“Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan siku tatu kabla ya kufariki dunia. Bado tunaandaa utaratibu wa kuaga mwili kisha kuelekea Morogoro kwa ajili ya maziko,” alisema Moses nyumbani kwao Kawe Avocado. 

Moses, ambaye ni mtoto mkubwa wa Liyumba, alisema marehemu baba yake ameacha watoto saba aliozaa na mke wake aliyefariki dunia mwaka 2005. 

“Tunasikitika kwa kifo cha mzee wetu, lakini ndiyo mapenzi ya Mungu. Watoto wake wote tupo, na wengine wawili wanaoishi nje ya nchi wameshafika kwa ajili ya kumpumzi- sha mpendwa baba yetu.” 

Mkurugenzi huyo wa zamani wa BoT aliandikwa sana kwenye vyombo vya habari mwaka 2009 alipokuwa anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi kati ya mwaka 2001 na 2006 wakati wa ujenzi wa majengo pacha ya makao makuu ya BoT. 

Siku ya hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya Sh221 bilioni lilitupwa, lakini alitiwa hatiani kwa shtaka la matumizi mabaya ya madaraka. Liyumba alitiwa hatiani Mei 23, 2010 kwa kosa hilo na kufungwa miaka miwili jela mpaka Septemba 24, 2011 alipoachiwa huru. 
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )