Monday, April 18, 2016

Oparesheni ya Kuwaondoa Ombaomba Jijini Dar es Salaam Yagonga Mwamba..... Polisi Wapanga Mikakati Mipya

OPERESHENI ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam imegonga mwamba kutokana na kukinzana na baadhi ya mamlaka katika kuwaondoa watu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kuondoa omba omba imeshindikana kutokana na baadhi ya mamlaka kushindwa kuhusishwa.

Amesema kuwa wanaendelea kujipanga kwa kuhusisha mamlaka zote ili kuweza kutekeleza operesheni hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuwa kuna omba omba wengine wameweza kuondoka baada ya tangazo kutolewa hivyo waliobaki waondoke kwa savabu operesheni itakayoanza haitaangalia uso wa mtu.

Jeshi Polisi limeweza kukusanya zaidi ya sh. Milioni 911 ambazo zimekusanywa kutokana na makosa mbalimbali ya magari  pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es Salaam.

Kamanda Sirro amesema kuwa hawajisifii kukusanya fedha hizo, nia yao ni kuona watu hawafanyi makosa ya usalama barabarani.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata jambazi sugu, Shaban Ramadhan (35) ambaye alikuwa anamiliki bunduki mbili za kivita SMG na risasi nane.

Kamishina Sirro amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa watu juu ya mtu huyo kumiliki silaha ambapo alikutwa na silaha moja huku moja ikiwa kwa rafiki yake wa kike, Fatuma Salehe (20).

Aidha jeshi la polisi limeonya wananchi kununua gari katika sehemu zinazotambulika  kutokana na kuibuka uhalifu wa watu kuuza gari zisizo kuwa zao.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )