Monday, April 4, 2016

Rais Magufuli Afuta Sherehe za Maadhimisho ya Muungano Mwaka Huu....Aagiza Fedha Zilizokuwa Zimetengwa Zitumike Kupanua Barabara ya Mwanza- Airpot


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.

Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )