Wednesday, April 20, 2016

Rais Shein Awaapisha Makatibu Wakuu Na Naibu Katibu Wakuu Wa (SMZ)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein jana aliendelea na hatua ya kuwaapisha makatibu wakuu wa wizara aliowateua juzi.

Walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Vuga mjini Zanzibar ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee na naibu wake, Salmin Amour Abdulla.

Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Radhia Rashid Haroub na Naibu katibu wake, Bushiri Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Asha Ali Abdulla na manaibu wake, Yakout Hassan Yakout na Kubingwa Mashaka Simba.

Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Joseph Abdalla Meza na naibu wake, Ahmed Kassim Haji.

Khamis Mussa Omar aliapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na naibu wake Ali Khamis Juma.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ni Bakari Haji Bakari, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Juma Malik Akili na naibu Halima Maulid Salum, Dk Jamal Adam Taib akiapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya.

Khadija Bakari Juma aliapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na manaibu wake, Abdalla Mzee Abdalla na Madina Mjaka Mwinyi.

Wengine ni Ali Khalil Mirza wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Juma Ali Jima wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na naibu wake, Maryam Juma Abdulla, Fatma Gharib Bilal, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na naibu wake Maua Makame Rajab.

Omar Hassan Omar, Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo na naibu wake Dk Amina Ameir Issa.

Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe na naibu wake, Shomari Omar Shomari. 

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )