Tuesday, April 5, 2016

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein amteua Hamadi Rashid kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi


Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua mwenyekiti wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi.


Uteuzi huo wa Rais Dkt Shein umefuata baada ya leo kutoa hotuba na kuzindua Baraza la wawakilishi ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na 
1.Mohamed aboud Mohamed
2. Amina Salum Ali 
3. Moulin Castico
4. Balozi Ali karume 
5. Said Soud Said na
6. Juma Ali Khatibu

Aidha uteuzi huo umeanza hii leo tarehe 05.04.2016.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )