Thursday, April 21, 2016

TAKUKURU Yalikana Tamko la Wakili wake Kwamba Mahakama ya Kisutu Imejaa Rushwa......Yasema Hayo Yalikuwa ni Maoni yake Binafsi


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU aliyenukuliwa kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na hali ya Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Wakili huyo alinukuliwa akisema kuwa “Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
 
Wakili Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si msimamo wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na jamii kwa ujumla itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake binafsi.
 
TAKUKURU ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni muhimili wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.
 
TAKUKURU inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake.

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO,
TAKUKURU MAKAO MAKUU
20 April, 2016

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )