Wednesday, April 27, 2016

Waziri Mkuu Majaliwa atembelewa na Waziri Viwanda wa Singapore Bungeni Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewakaribisha wafanya biashara kutoka nchini Singapore kuja kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo mjini Dododma alipokuwa akiongea na Ujumbe wa Singapore ulioongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda Mhe. Kol Poh Koon aliyeambatana na wafanyabiashara mashuhuri kujifunza na kujionea fursa zilizopo nchini katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa anaamini kampuni za Singapore zitakazowekeza nchini zitakuwa na tija katika sekta ya mafuta na gesi asilia, kilimo, Uchukuzi pamoja na Viwanda katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kuhusu kuimarika kwa ushirikiano kati Tanzania na Singapore, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inawajengea uwezo watumishi wake katika kada za uhandisi, sheria na wachumi ambao watakuwa msaada mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi inayokua nchini ambapo Singapore wamepiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda kutoka nchini Singapore Mhe. Dkt. Kol Poh Koon ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na nchi yake huku akionesha kuridhishwa kwake na uhusianao mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Waziri huyo wa Biashara na Viwanda kutoka nchini Singapore amesema kuwa nchi yake itatoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania katika kuhakikisha inawajengea uwezo watendaji wakuu wa Serikali ili Tanzania iweze kufikia malengo waliojiwekea katika kuwahudumia wananchi wake.

Aidha,   awali akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Medalled Karemaligo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa nchi yake itatumia rasilimali walizonazo ikiwemo rasilimali watu kuwafundisha wataalamu kutoka Tanzania ili waje kuwafundisha wataalamu wengine hapa nchini kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Kuhusu Bandari ya Dar es salaam, Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa bandari hiyo ni nzuri ikilinganishwa na bandari nyingine zilizopo katika ukanda wa Bahari ya Hindi kwa kuwa ipo karibu zaidi na Singapore hali ambayo itarahisisha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Katika kuonesha nchi yake inavyojali ushirikiano na Tanzania, Mhe. Dkt. Kol amemkaribisha Waziri wa Nishati na Madini kwenda kushiriki wiki ya nishati nchini Singapore ambayo huadhimishwa Oktoba kila mwaka.

Ujumbe huo kutoka nchini Singapore upo nchini kwa muda wa siku tano kuanzia Aprili 26 hadi 30, 2016 ambapo wanatembelea maeneo mbalimbali ya ikwemo Dar es salaam, Dodoma na mkoa wa Morogoro ambapo watazindua mradi wa ushirikiano utakaojulikana kama “Star City”.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (katikati) leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Singapore nchini Tanzania.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )