Wednesday, April 27, 2016

Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atoa Onyo kwa Wasimamizi wa Elimu

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewatahadharisha kuwawajibisha maafisa elimu wa shule za msingi watakaoshindwa kusimamia elimu na kusababisha wanafunzi wamalize shule za msingi bila kujua kusoma na kuandika.

Prof. Ndalichako amesema hayo Mjini Iringa katika mafunzo ya wakaguzi na wadhibiti wa ubora wa elimu mashuleni kutoka wilaya 31 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Prof. Ndalichako amesema kuwa ni aibu kwa wanafunzi waliosoma miaka saba darasani hawajui kusoma na kuandika wakati Wakaguzi na Wasimamizi wa Elimu wapo katika maeneo husika na kuwataka wajitathimini kama wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.

Waziri huyo pia amewataka wadhibiti hao wa elimu kufanya ukaguzi wa vitabu na vifaa vya kufundishia vikiwa na ubora unaokubalika huku akiahidi kuzingatia mahitaji ya walemavu katika shule za serikali.

Kwa upande wao walimu pamoja na wadhibiti hao wa elimu wameiomba serikali kushughulikia madai yao na kuboresha mazingira ya kufanyika kazi ikiwemo pamoja na fungu la kutosha na kuendeshea ukaguzi wa elimu.
Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.
Mkuu wa mkoa Bi.Amina Masenza akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Ndalichako,Bi Masenza alimuomba waziri wa Elimu kuhakikisha Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania.
Baadhi ya waliohudhuria mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyofanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. Mafunzo hayo yajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )