Tuesday, May 10, 2016

Chadema Kuijadili Serikali ya Rais Magufuli


Kamati Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 11 Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene imesema kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kitajadili taarifa ya hali ya siasa nchini.

Pia kikao hicho kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama kwa mwaka huu unatokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5 kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji.

Mpango huo utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )