Wednesday, May 11, 2016

Jeshi La Wananchi ( JWTZ ) Kuendelea Kupewa Mafunzo Ili Liwe Kisasa Zaidi


Na Tiganya Vincent,  MAELEZO--Dodoma
Wizara ya Ulinzi na Kujeshi la Kujenga Taifa imepanga kuendelea kuliimarisha na kuliongezea uwezo Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania kwa kulipatia vifaa na zana za kisasa pamoja na kutoa mafunzo stahiki ili kuwa tayari kukabiliana na adui wa ndani na nje.

Mpango wa Serikali umetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh.Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akiwasilisha hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.

Alisema kuwa sanajari na hili , Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa Wanajeshi nchini ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma na mahitaji ya msingi kama vile chakula , tiba, sare , usafiri na stahili zao.

Mh. Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa Wizara itaimarisha uwezo wa Jeshi katika utafiti na kuendeleza teknolojia kwa madhumuni ya kuisaidia uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia hapa nchini na nje ya nchi.

Aidha , alisema kuwa Wizara kupitia Jeshi la Kujenga la Taifa itaendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya uzalendo , umoja wa Kitaifa , ukakamavuna kuwapatia stadi za kazi ili kuwaandaa katika uzalishaji mali.

Dkt. Mwinyi alisema Wizara kupitia Jeshi litaendelea kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiulinzi na nchi nyingine duniani kupitia Jumuiya za Kimataifa , Kikanda na ushirikiano na nchi moja moja.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husein Ali Mwinyi ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla shilingi trilioni 1.7 (1,736,530,413,000.00) kwa ajili ya matumizi ya kawaidia na matumizi ya maendeleo.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi trilioni 1.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na bilioni 248 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )