Tuesday, May 3, 2016

Kesi Kitilya na Wenzake Yaahirishwa tena mpaka Mei 18


Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam inatarajia kuanza kusikiliza rufaa ya kupinga kufutwa shtaka la nane katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili, mei 5, mwaka huu.
 
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya mahakama hiyo kuitisha jalada halisi la kesi hiyo la kujipatia dola milioni 6 za marekani, aprili 29.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mrembo wa  Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic, Sioi Solomon.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro aliieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, mbele ya hakimu Mkuu Mkazi  Mh. Emmillius Mchauru, kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, hakimu Mchauru alisema alitarajia kutoa mwenendo wa kesi hiyo, lakini amepokea taarifa kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kwamba washtakiwa wanatakiwa kufika mahakamani huko.

Hakimu Mchauru alisema kutokana na taarifa hiyo aliyopokea kutoka kwa viongozi wake wa juu, washtakiwa na mawakili wao hawana budi kufika mahakama kuu ili kujua nini kitajiri.

Mawakili wanaowatetea washtakiwa hao ni Dk.Lingo Tenga, Majura Magafu na Alex Mgongolwa.

Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi mei 18, ambapo alisema washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu kama taratibu za kisheria zinavyosema, licha ya kuitwa mahakama kuu.

Hata hivyo, baada ya kufika mahakama kuu, Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alisema suala ambalo lipo mbele yake linahusu taarifa ya pendekezo la kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufutwa shtaka la nane la utakatishaji fedha lililowasilishwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Shtaka hilo la utakatishaji fedha inadaiwa watuhumiwa wote kwa pamoja  kati ya march 2013 na septemba 2015 Jijini Dar es Salaam walitakatisha fedha dola za kimarekani milioni sita kwa kuzihamisha kutoka katika akaunti ya kampuni ya Egma  zilizokuwa zimefunguliwa benki ya Stanbic tawi la Tanzania kwa namba mbalimbali.

Jaji Mzuna alisema kutokana na uwepo wa taarifa hiyo mezani kwake, pande zote mbili zinapaswa kufika siku ya alhamis mei 5, mwaka huu kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa rufani.

Pia alisema licha ya kupanga tarehe hiyo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, endapo kama upande wa Jamhuri haujawasilisha hati ya rufani katika muda uliotolewa, basi itatolewa taarifa ya mwenendo wa kesi hiyo.

Baada ya kutoa maelezo hayo, wakili Magafu aliieleza mahakama kwamba wanakubaliana na hatua hiyo, licha ya kuwa upande wa Jamhuri haukufika mahakamani hapo.

Uamuzi wa kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha, ulitolewa na hakimu Mchauru baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi  kwamba halijakidhi vigezo vya kisheria.

Hata hivyo, uamuzi huo ulipingwa baada ya Jamhuri kupitia wakili mkuu wa serikali, Oswald Tibabyekomya kudai kuwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kusudio la mapendekezo ya kukata rufaa
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )