Monday, May 16, 2016

Kiwanda Cha Bia Serengeti Breweries Limited (SBL) Chapigwa Faini

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga Mpina amekiamuru Kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL), kulipa faini ya Sh16 milioni kwa kosa la kutiririsha maji yasiyo salama kwenye makazi ya watu.

Uamuzi huo ulichukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya baadhi ya viongozi wa SBL kilichopo Chang’ombe Manispaa ya Temeke na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), baada ya kujiridhisha kuwa kilikiuka taratibu za utunzaji mazingira na kutotekeleza amri halali kwa zaidi ya miaka miwili.

Mpina aliigiza kiwanda hicho, kulipa faini ndani ya siku saba na kwamba asieleweke vibaya kuhusu uamuzi huo, bali anasimamia sheria.

“Nasimamia sheria wala sina nia mbaya na kiwanda chenu, naomba nieleweke hivyo na faini hii mlipe kwa wakati,” alisema Mpina.

Mkurugenzi Mkuu wa Nemc, Bonaventure Baya alisema baraza hilo limejijengea utaratibu wa mara kwa mara kufuatilia kanuni za afya za kiwanda hicho hasa majitaka yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.

Meneja Mhandisi Biashara wa SBL, Peter Mkongwa alikanusha tuhuma hizo na kwamba, maji hutibiwa kwa dawa kabla ya kutiririshwa katika makazi ya watu. Alisema: “Tunasubiri mashine maalumu ya kuvuta maji hayo ili yaingie katika bomba.”

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )