Friday, May 13, 2016

Maadhimisho Ya Miaka Sita Ya Chama Cha Watanzania Waliosomea China (CAAT)


Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6 (2010-2016) tokea kilipozaliwa.

Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu  Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 kuanzia saa 8 alasiri.

Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa China.

Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China.

Kwenye sherehe hiyo pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT. Baada ya chakula cha pamoja cha jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara, wajasiliamali na wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma wanazotoa.

Dhima kuu ya tukio hilo ni:
•Utambulisho wa jumuia ya CAAT ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo yao katika Jamhuri ya Watu wa China
•Kubaini na Kuainisha fursa zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT
•Maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za biashara za wanajumuia.

Wote mliopata kusoma China mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio.

Unaweza kushiriki kwa kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au emailgsoreku@yahoo.com

Asante
 George Oreku
Katibu Mkuu
Chama cha Watanzania Waliosoma China (China Alumni Association of Tanzania)
05-May-2015
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )