Tuesday, May 10, 2016

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Ajisalimisha Polisi, Ahojiwa Kwa Masaa 6


Polisi wilayani Arumeru jana iliwashikiliwa kwa muda mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na madiwani 35 wa Chadema kwa tuhuma za kuvamia eneo na kuharibu mali.
 
Viongozi hao, wiki iliyopita walivunja uzio wa mabati uliojengwa jirani na halmashauri na mfanyabiashara Itandumi Makere, wakimtuhumu kupata eneo hilo la Serikali kinyume cha sheria.
 
Nassari na madiwani hao, walishikiliwa kwa muda baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Usa River. Viongozi hao, baada ya kufika polisi saa tatu asubuhi walihojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma hizo.
 
Nassari alisema kitendo hicho cha kufikishwa polisi na kuhojiwa hakiwatishi kwani wanachokifanya ni kutetea ardhi ya Wameru.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Wille Njau alisema wamedhalilishwa na hatua hiyo kwani walikuwa wanatekeleza uamuzi ya Baraza la Madiwani.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kuhojiwa kwa mbunge na madiwani hao na kusema wanafanya uchunguzi na jalada litawasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )