Sunday, May 29, 2016

Mtoto Wa Miaka 4 Afariki Dunia Baada Ya Kuungua Kwa Moto Ndani Ya Nyumba Yao Jijini Mwanza

MTOTO Vestina Masolwa (4) wa kitongoji cha Nyamungu– Mwabagole katika kata ya Mwangalangha tarafa ya Ndugu wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, amefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto jikoni wakati nyumba yao ikiteketea kwa moto.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 9 alasiri katika kitongoji hicho, baada ya mama wa marehemu, Grace Wilson (30), kupika chakula na kisha kwenda shambani nje kidogo na nyumba hiyo akiwa amemuacha mtoto huyo jikoni.
 
Kwa mujibu ya taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema baada ya mama huyo kwenda shambani na kumuacha mtoto wake (marehemu), alianza kuchezea moto uliosababisha nyumba yao kuungua.
 
“Wakati mama wa marehemu akiwa anaendelea na shughuli zake shambani, aliona nyumba yake ikiungua moto na kuamua kukimbia kurudi nyumbani na kukuta nyumba ikiteketea na kusababisha mtoto Masolwa kufariki dunia papo hapo."
 
Kamanda Msangi alisema mwili wa marehemu tayari ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi, lakini chanzo cha tukio hilo likidaiwa ni uzembe wa wazazi kushindwa kuwa waangalifu kwa mtoto huyo na kusababisha kifo na nyumba kuungua.
 
Hata hivyo, alitoa wito kwa wazazi wawe makini na waangalifu wakati wote na watoto ili kuwaepusha na ajali zinazoweza kuepukika, huku pia akiwataka kuhakikisha kabla hawajaondoka kwenda kwenye shughuli zao za kila siku, wanawaacha watoto wao kwenye mazingira salama.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )