Wednesday, May 11, 2016

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atoa Ushauri Wa Kupunguza Foleni Dar es Salaam


Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutekeleza mipango iliyowekwa na serikali yake endapo atahitaji kumaliza na msongamano katika jiji hilo.

Kikwete alitoa ushauri huo jana, alipotembelea Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, huku akionyesha kuridhishwa nalo na kumtaka Makonda kuweka historia kama mkuu wa mkoa kijana kumaliza msongamano.
 
Alisema kuna mipango ambayo iliwekwa na serikali ya awamu ya nne katika kumaliza msongamano huo, ikiwamo uboreshaji wa reli ili kubabiliana na tatizo la usafiri, uboreshaji wa stendi za mabasi ya kwenda mikoani za Boko, Pugu na Mbezi Luis, ambavyo alisema ni muda mrefu sasa haoni utekelezaji wake.
 
“Kwa mfano kuna ile stendi ya Boko na mingine ni mipango ambayo iliwekwa lakini naona imekaa muda mrefu hakuna utekelezaji wake. Naona tu unakwenda unarudi, unakwenda unarudi, ” alisema.
 
Kikwete alisema hakuna uchawi utakaosaidia kumaliza msongamano katika jiji la Dar es Salaam pasipo kuboresha huduma za msingi katika makazi yaliyoko pembezoni mwa mji huo pamoja kutumia treni.
 
Alisema jiji la Dar es Salaam linahitaji usafiri ambao utachukua idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja na kutolea mfano baadhi ya maeneo ya Ubungo, Tazara, na Mwembechai kwamba endapo yangewekwa reli na treni ikaanza kutumika, ingepunguza idadi ya magari binafsi barabarani.
 
Alisema pamoja na kuanza kwa mradi wa mabasi ya mwendo kasi, bado kunahitajika usafiri wa treni katika jiji, ambao alisema ukiboreshwa vizuri utawavutia hata wa wa maisha ya kawaida kuutumia na pia na kuacha magari yao nyumbani.
 
“Tatizo kubwa la Dar es Salaam wakazi wengi wanapata huduma katika eneo moja, yapo maeneo ya Mabwe Pande, Kigamboni na mengine ya pembezoni. Yatumieni vizuri, wekeni huduma huko, jengeni maduka, osifi na huduma muhimu huko. Sisemi mhamishie huko ofisi za serikali lakini huduma ziingine muhimu ili yule atakayetaka kuja mjini awe amependa mwenyewe,” alisema.
 
Makonda alisema amapokea ushauri huo na ataufanyia kazi na kuongeza kwamba iko mipango mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kupunguza kero mbalimbali katiika jiji hilo.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )