Friday, May 13, 2016

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Kwa Vyombo vya Habari


Mwanamke mmoja amejeruhiwa kwa kukatwa na panga kwenye bega la mkono wa kulia wilayani sengerema.

Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni wezi walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa mbao silvia oscar na kujeruhi watu wawili huko igombe wilayani ilemela.

Katika tukio la kwanza.
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la juliana mashiko miaka 41 mkulima na mkazi wa kijiji cha kizugwangoma alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kwenye bega la mkono wa kulia na mathias saliana miaka 19 hali iliyopelekea kurupushani na yowe akiomba msaada kutoka kwa majirani ili waweze kumsaidia. 


Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 13.05.2016 majira ya 02:30hrs katika kijiji na kata ya kizugwangoma wilaya ya sengerema mkoa wa mwanza.

Inadaiwa kuwa mathias saliana alikwenda nyumbani kwa bi juliana akiwa na panga akidai apewe fedha kwa lazima huku mwanamke huyo akigoma nakuamua kumkata panga bi juliana kwenye bega la mkono wa kulia ndipo mwanamke huyo alianza kupiga yowe akiomba msaada kutoka kwa majirani, ndipo majirani walifika na kumsaidia mama huyo.

Aidha baada ya kumsaidia bi juliana, wananchi hao walimkamata kijana huyo na kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha wakamfikisha kwenye kituo cha polisi akiwa na hali mbaya kiafya na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya misheni ya wilaya ya sengerema akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake katika kupambana na uhalifu katika mkoa wetu wa mwanza. 


Lakini pia akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi bali watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapomkamata mhalifu ili aweze kufikishwa polisi na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria ili iwe mfano kwa watu wengine.

Katika tukio la pili.
Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni wezi walivamia nyumbani kwa mfanya biashara wa mbao wa kigote – igombe anayejulikana kwa jina la bi Silvia Oscar miaka 30 na kumjeruhi kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kwenye kiganja cha mkono wa kushoto, akafanikiwa kujiokoa kwa kukimbia na kuwaacha watu hao ndani ya nyumba. 


Ndipo walipokutana na baba mzazi wa Silvia anaeishinae hapo nyumbani kwake aitwaye Oscar Mkaima miaka 57 ambaye walimjeruhi kidogo kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani. 

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12.05.2016 majira ya saa 20:40hrs usiku katika mtaa wa kitoge- Igombe kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Inadaiwa kuwa wahalifu hao waliingia ndani ya nyumba hiyo na kuwakuta wenye kaya wakiwa wanakula chakula, hawakuchukua kitu chochote. 


Majeruhi wametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano dhidi ya tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amesema jeshi la polisi linafanya msako mkali wa kuwatafuta watu waliohusika kwa namna moja au nyingine kwenye tukio hilo na kuhakikisha wanakamatwa, pia ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wahalifu au uhalifu mapema ili wahalifu wawezwe kukamatwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyo elekeza.

Imesainiwa na. 

Sacp: Ahmed Msangi

Kamanda wa Polisi (m) Mwanza

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )