Friday, May 6, 2016

Wabunge Wanawake wa UKAWA watoka nje ya Bunge baada ya Mbunge wa CCM Kuwatuhumu Kwamba Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi na Viongozi Wao

Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga (CCM ) aliyedai jana kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.

Mlinga alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia hotuba Wizara ya Katiba na Sheria  ambapo alisema ili uweze kuwa mbunge wa viti maalum chadema, lazima ufanye mapenzi na kiongozi wako wa chama.
 
Wabunge hao leo asubuhi  waliomba mwongozo kwa Naibu Spika 
kupitia kwa Mbunge Sophia Mwakagenda wa viti maalumu (Chadema) kumtaka mbunge huyo athibtishe kauli yake  lakini hawakusikilizwa na badala yake Naibu spika aliwataka wakae chini.

Baada ya mabishano ya dakika kadhaa pasi kusikilizwa, wabunge hao  walisimama wote na kuamua kutoka nje  ya ukumbi wa bunge huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa.
 
==>Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge hao kutoka nje

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )