Tuesday, June 7, 2016

Rais Magufuli amteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji KiongoziRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

07 Juni, 2016

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )