Friday, July 1, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Saba

Mtunzi:  Enea Faidy


.....DOREEN alimkubalia Eddy kuwa mpenzi wake lakini alimweleza kuwa kuna sharti ambalo Eddy lazima alifuate ndipo awe nae.Dorice hakutaka kukubali kirahisi kumwachia Doreen kuwa na Eddy hivyo alipanga kulipiza ili Doreen asije kumsahau.Mwalimu John alipigwa na mkewe mpaka akapoteza fahamu ambapo mkewe alichanganyikiwa sana baada ya kumwamsha bila mafanikio....

Endelea.....
...MWALIMU JOHN alikuwa kimya pale kitini akiwa hana fahamu yoyote, mkewe akazidi kuchanganyikiwa sana kwani alihisi tayari mumewe ameaga dunia.

"Jamani mume wangu amka bado nakupenda! Nisamehe Mimi John wangu!" Alizidi kulia mke wa mwalimu John kwa huzuni na majuto makali. Alijiona mjinga sana kwa kujichukulia maamuzi mkononi bila hata kumdadisi vizuri.

Simanzi ilimtanda mwanamke yule bila kujua la kufanya, machozi yalichuruzika kama mito miwili usoni kwake kwani ndio kwanza ndoa yao ilikuwa changa kabisa tangu waoane miezi mitano iliyopita sasa iweje John aage mapema kiasi hicho? Mkewe aliufikiria upweke ambao angekabiliana nao Siku za usoni. Huzuni ikamzidia.

Mwalimu John akiwa bado ameyafumba macho yake akahisi yumo kwenye usingizi mzito sana lakini alikisikia vyema kilio cha mkewe.

Alitamani aamke ili amtulize mkewe lakini mwili ulikuwa kama umegandishwa na sumaku. Hakuweza hata kutikisika, ghafla akahisi upepo mkali sana ndani ya nyumba yake alipotazama ukutani akakutana na sura ya kutisha sana.

Huku ikifuka moshi mdomoni, macho mekundu kama damu na kichwani yalichomoza mapembe mawili marefu. John aliogogopa sana kwani tangu azaliwe hakuwahi kukutana na kiumbe wa ajabu na wakutisha namna ile. Alitamani azinduke usingizini lakini hakuweza, hivyo alibaki akitetemeka.

Ghafla kiumbe yule akabadilika na kuwa sura ya msichana mrembo sana. Mwalimu John akabaki kinywa wazi akistaajabu ya Mussa. Alipotazama vizuri aligundua ni Doreen , akashtuka sana.Doreen alimtazama mwalimu John kwa dharau sana kisha akaachia kicheko kikali sana.

"Mimi ni Doreen Mbwana! Daima usinichezee maana sichezewi kirahisi.. Unataka kuniendea Malawi we? Hahahahah umechelewa sana John, nina nguvu kuliko unavofikiria"

Doreen akamsogelea John, na kutoa kucha zake ndefu nyembamba kama msumari kisha akamgusa mdomo John."Umeniita Nimekuja! Sasa utaipata fresh...! Hahahahahahahhh" alisema Doreen kisha akatoweka . John alihema kwa nguvu sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani maneno ya Doreen yalimtisha.

==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )