Wednesday, June 1, 2016

Shein: Hakuna Mtu Wala Nchi Yakuweza Kuniondoa Madarakani

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema hakuna nchi au jumuiya za kimataifa zitakazomwondoa madarakani yeye kwa sababu amechaguliwa kihalali na wananchi kwa kura nyingi kwa mujibu wa Katiba.

Dk Shein alisema hayo wakati akizungumza na wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika matawi ya Wesha Tibirinzi, Pembeni Shengejuu na Maziwa Ng’ombe, Micheweni katika ziara ya kuwafariji kutokana na matukio ya hujuma zilizofanywa na wapinzani huko Pemba.

Aliwataka wafuasi wa CCM na wanachama wake waliopo Pemba, wasibabaishwe na kauli zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa wanaopita na kudai kwamba uchaguzi mwingine unakuja.

“Mimi ndiye Rais halali wa Zanzibar nimechaguliwa katika uchaguzi ulioitishwa na Tume ya Uchaguzi... wananchi msisikilize uvumi na kauli za wapinzani zenye lengo la kuwababaisha na kuwayumbisha katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Dk Shein.

Dk Shein alisema amesikitishwa na kauli za uchochezi zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa zenye malengo ya kuishawishi jamii kutengana na kugombana na kususiana hata katika shughuli za jamii ikiwemo misiba.

Alisema kiongozi anayefanya vitendo vyenye lengo la kuwagawa wananchi kwa malengo ya kisiasa  huyo ameishiwa na hana nafasi katika jamii. 

“Huyo kiongozi anayewashawishi wananchi kususia shughuli za jamii na maendeleo basi huyo ameishiwa kisiasa na hana nafasi katika jamii ya wananchi na ninyi mpuuzeni.Alikuwa na nafasi ya kushiriki katika uchaguzi lakini alisusa,” alieleza.

Alisema viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wameishiwa hoja kwa sasa na hawana la kufanya baada ya kugomea kushiriki katika uchaguzi halali wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu ambao umetoa nafasi kwa CCM kushinda katika uchaguzi wa kishindo.

Mapema Dk Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM aliwataka wanachama wa chama hicho kutembea kifua mbele na kuachana na unyonge kwa sababu chama chao ndiyo kilichoshika dola na kuunda serikali.

Akizungumzia yanayotokea Pemba, Dk Shein alisema, “Nimesikitishwa na taarifa za matukio mbalimbali yanayofanyika huku Pemba ikiwemo watu kususiwa maiti, kushushwa katika gari za abiria baada ya kuwa na itikadi tofauti......haya matukio hayakubaliki na yanakwenda kinyume cha maamrisho ya dini zote.”

Aliwataka viongozi waliopewa majukumu kwa mujibu wa Katiba kufanya kazi zao na kupambana na vitendo vya ubaguzi ikiwemo vya kuonewa kiholela wananchi.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )