Saturday, July 30, 2016

Bomba la mafuta Kutoka Uganda Hadi Tanga lahujumiwa.....Wananchi Waanza Kuvamia Ili Walipwe Fidia


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), amewaonya wananchi wanaotaka kuvamia njia, litakapopita bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga, kwa kujenga nyumba ili kulipwa fidia mradi utakapoanza.

Aliwaeleza kuwa bomba hilo lililopewa jina la East Africa Crude Oil Pipeline, watakaovamia wanapoteza fedha zao na itakula kwao, kwani watatumia ramani ya satelaiti iliyopigwa Juni mwaka jana, muda ambao mazungumzo ya ujenzi wa bomba hilo yalianza.

Akizungumza katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara zote pamoja na wakuu wa mikoa ambao bomba hilo linapita, Muhongo alieleza kuwa watu hao hawawezi kudanganya kwa lengo la kupata fedha wakidai kuwa bomba limewakuta.

Alisema kuna satelaiti 1007 zinazofanya utafiti duniani na mpaka Agosti mwaka jana, zilikuwa zote zikifanya kazi hivyo kuonesha ni majengo gani yalikuwepo katika njia hiyo, hivyo kutaka wananchi wapewe ramani inayoonesha bomba litakapopita ili kuepusha gharama.

Muhongo alisema leo atakutana na waziri wa Nishati wa Kongo kwa lengo la kujadiliana jinsi nchi hiyo itakavyoshirikishwa kwenye mradi huo mapema, huku akitarajia nchi ya Burundi kuungana katika mradi huo.

Alisema hatua hiyo itawezesha bomba hilo kutumiwa na nchi hizo kupitisha mafuta.

Burundi na Tanzania zinaendelea na utafiti katika ziwa Tanganyika na yakipatikana watatumia bomba hilo. Muhongo alisema pia wanatarajia kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta kutoka Sudani kusini kutokana na kuwa ni rahisi kuyasafirisha mpaka Uganda na kutumia bomba hilo.

Bomba hilo la mafuta linatara kutumia Dola za Marekani bilioni 3.5 mpaka litakapokamilika na kutaka katibu mkuu kuunda kamati maalumu ya kudumu ambayo itakuwa na wajumbe wawili au watatu kutoka kila wizara kuhakikisha mradi huo unakamilika.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )