Wednesday, July 20, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 17

Mtunzi: Enea Faidy

..... MANSOOR alimtazama Dorice kwa jicho la kiulizo lililomtaka azungumze chochote lakini Dorice hakusema neno zaidi ya kuangua kilio cha huzuni baada ya kukosa msaada kwa Mansoor. Dorice alilia sana kwani alijua kurudi tena duniani sasa ni ndoto.

"Mansoor naomba unisaidie!" Dorice alipiga magoti akamsihi Mansoor aweze kumsaidia ili arudi kwao pia amsaidie kumwokoa Eddy ili furaha ya penzi lake irudi.

"Dorice! Naweza kukusaidia kwa yote hayo... Ila inabidi ukubali kuolewa na Mimi maana bila hivyo mama yangu hatonielewa...!" Mansoor alisisitiza.
"Siwezi kuolewa na wewe..!"

"Kwanini? Au kwa vile Mimi sio binadamu mwenzio? Jua nakupenda na nitakuruhusu kuendelea na Eddy.. Nielewe Dorice!" Mansoor alizidi kumweka Dorice katika wakati mgumu sana kwani kiukweli Dorice aliuhitaji msaada wa Mansoor ila masharti yake yalikuwa kikwazo sana. 

Dorice alishindwa kung'amua juu ya mtihani ule mzito. Alijua fika wazazi wake wataumia sana endapo wakijua kuwa Hayupo duniani, aliyafikiria maumivu ambayo mama yake angeyapata kama yeye angepotelea kule kwenye ulimwengu wa majini.

"Sijui nimkubali halafu akinirudisha duniani nimkatae?" Dorice Alizidi kuwa na utitiri wa mawazo kichwani mwake. Ghafla akashtushwa na sauti nzuri ya mahaba ya Mansoor akizidi kumshawishi kuwa amkubalie ili aweze kumsaidia kutatua matatizo yake.

"Dorice! Nifanye nifurahi tafadhali.. Nilipendwa na wengi ambao si chaguo langu.. Nasikitika chaguo langu linakuwa mwiba moyoni mwangu! Kwanini lakini?"

Dorice alivuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu, huku akiwa ameinamisha kichwa chake. Taratibu akanyanyua kichwa chake na kumtazama Mansoor. Macho yake yalistaajabu uzuri wa asili aliokuwa nao kijana yule. Hata kama majini ni wazuri lakini Mansoor alizidi kipimo, kuanzia macho yake, pua yake na midomo mizuri ya kupendeza sana.

"Nimekubali Mansoor! Ila kabla ya yote naomba uniahidi kama utanisaidia!" Alisema Dorice kwa sauti iliyotulia sana. Maneno hayo yalifungua ukurasa mpya moyoni kwa Mansoor, alifurahi kupita kiasi akamkumbatia kwa nguvu Dorice.

"Nakuahidi kukusaidia Dorice!" Alisema Mansoor akiwa amemkumbatia Dorice.
Walikumbatiana kwa muda kisha wakaachiana. Mansoor akamtazama Dorice huku akitabasamu.
"Nataka uvae vizuri nikupeleke kwa mama yangu muda huu!"
"Nitavaa nini? Sina nguo!"
Alisema Dorice kwa woga huku moyo wake ukimsuta kwa kumsaliti Eddy kwani alikwisha muahidi kuwa hatokuwa na mwanaume mwingine yeyote zaidi yake."lakini ni kwa sababu yake..!" Alijipa Jibu Dorice.
"Unapenda nguo gani?" Aliuliza Mansoor.
"Nguo yoyote itakayonifaa!" Alijibu Dorice.

Mansoor alinyoosha mkono juu ghafla ukatokea mfuko mmoja wenye ukubwa kiasi kisha akamkabidhi Dorice. Dorice aliogopa sana, akasita kupokea.
"Usiogope.. Chukua!"
Dorice akapokea mfuko ule japo kwa woga kisha akaufungua ili atazame kilichomo. Akapigwa na bumbuwazi.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )