Sunday, July 24, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 19


.....DORICE alipozitazama zile nguo zilikuwa ni nguo nzuri sana za kuvutia. Kulikuwa na gauni moja refu linaloacha wazi mikono lenye rangi ya dhahabu inayong'aa sana. Kulikuwa na viatu virefu vinavyoelekeana na rangi ya gauni kidogo, ushungi wenye rangi ya gauni, mkufu wa dhahabu pamoja na hereni.

Dorice alivishangaa vitu vile kwa mshangao wakati huo Mansoor alikuwa akiachia tabasamu mwanana pembeni yake.

"Vaa Dorice!" Ilisikika sauti ya Mansoor ndipo Dorice alipopata nafasi ya kumtazama tena Mansoor. Akapigwa na bumbuwazi baada ya kuona mansoor amevalia nguo tofauti na alizokuwa amevaa mwanzo, alionekana kama mwanaume wa kihindi pale anapofunga ndoa kwa mavazi yake. Dorice alimshangaa sana Mansoor, woga kiasi ukamvaa moyoni mwake kisha akaanza kuzivaa nguo zile alizopewa na Mansoor.

Pindi anapozivaa nguo zile Mansoor alikuwa tayari ameshatoweka eneo lile.Dorice alipovaa nguo zile, alibadilika sana. Alionekana mrembo mno kwa jinsi alivyopendeza. 

Ukimtazama kwa haraka utadhani msichana kutoka India kumbe ni mnyaturu wa Singida. Alijitazama kupitia kioo kilichokuwa mbele yake, akajikiri kwamba kweli Mungu hakumkosea katika uumbaji ila alitumia ufundi wa hali ya juu katika kukamilisha sura na umbile lake.

Bada ya kumaliza kuvaa, Mansoor alitokea tena palepale alipokuwa amesimama mwanzo. Alimshtua sana Dorice lakini tayari alikuwa ameshaanza kumzoea Mansoor hivyo hakuogopa sana.

"Umependeza sana Malkia wangu.. Kwa jinsi ulivyo sitamani hata uende Duniani.. Nahisi wivu sana.." Alisema mansoor huku akimtazama mrembo yule kama waridi likiwa bustanini wakati wa jua la asubuhi.

"Uliniahidi nini?" Aliuliza Dorice kwa hamaki."Usijali... Nitakupeleka duniani kama nilivokuahidi ila nimekuambia tu hisia zangu... Kama unanipenda kweli ni heri ubaki na mimi huku huku kwetu!" Alisema Mansoor kwa sauti ya upole sana. Dorice hakijibu kitu. Wakaondoka pale na kwenda moja kwa moja kwa malkia.

Malkia alifurahi sana kuona kijana wake ameambatana na mtu ampendae. Radi tatu mfululizo zilipigwa ili kudhihirisha furaha aliyokuwa nayo malkia. Mansoor alitabasam akiwa amemshika mkono mkewe mtarajiwa.

"Harusi ya mwanangu Mansoor... Iwe ya furaha sana kwani amepata kile alichokuwa anahitaji.." Alisena malkia kwa sauti kali. Dorice alimtazama Mansoor kwa woga.

"Usiogope malkia wangu.. Na kuanzia Leo nitakuita Aisha..!"
"Aisha! Kwanini?" Alihamaki Dorice.
"Ukiwa mke wangu huwezi kuitwa Dorice.." Alisema Mansoor.

Wakati Dorice akiendelea kushangaa ghafla upepo mkali ukapigwa, halafu kwa muda huohuo walijikuta wapo eneo lingine lililojaa watu wengi ambao Dorice hakuwaelewa elewa kwa jinsi walivyokuwa.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )