Thursday, July 28, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 21


Mtunzi: Enea Faidy
... MR ALOYCE alichanganyikiwa sana baada ya kukuta damu ikiwa imetapakaa sakafuni chumbani kwa mwanaye. Alipigwa na butwaa huku hofu ya kuondokewa na mwanae ikiwa imemvaa ghafla.

"Eeeddy!" Alijikuta anaita kwa sauti Kali ili kama Eddy yupo mbali asikie na aitikie wito ule ambao ungemwondolea wasiwasi Mr Alloyce. Lakini wito ule haukuitikiwa na mtu yoyote zaidi ya ukimya uliokuwa umetawala ndani ya jumba lile la kifahari.

Mr Alloyce alijaribu kuita tena na tena lakini bado hakuitikiwa. Simanzi ikamjaa tele, akajua tayari amepata pigo lingine zito kabla hata kidonda cha mwanzo hakijapona kwani ndio kwanza kilikuwa kibichi.

"We Mungu wangu nimekukosea nini Mimi mbona unaniadhibu hivi? Nihurumie uikomboe familia yangu" alilia mr Alloyce akiwa amejibwaga sakafuni kwenye korido ya kuelekea sebuleni. Machozu yalimchuruzika kama mvua huku yakiteremka kama vijito kuelekea kwenye marumaru za rangi ya maziwa zilizochanganyika na weupe.

"We Mungu nitaishi vipi Mimi na upweke huu? Sina mke, sina mtoto?" Alilalamika kwa majonzi mr Alloyce. Aliwaza mengi sana yaliyozidisha simanzi yake moyoni, moyo wake ukajawa na maumivu makali sana kama mtu aliyechomwa na mkuki wa moto katikati ya moyo wake.

"Bora na Mimi nife kuliko kubaki kwenye hali kama hii...!" Aliwaza Mr Alloyce kisha akainuka pale sakafuni na kuelekea chumbani kwake. Aliingia chumbani na kuwasha taa, kisha akaisogelea droo ya dressing table akaifungua na kuanza kupekuapekua vitu.

Alipekua kwa muda kisha akapata karasi ya ranging ya kaki akafunua kwa umakini kisha akazikuta dawa alizozihitaji. Kulikuwa na vidonge Vingi sana ndani ya pakiti ile kaki, akavibeba na kuirudisha droo kama ilivyokuwa akatoka kuelekea sebuleni.

Alifika sebuleni na kuliendea jokofu ili achukue pombe Kali anywe pamoja na vile vidonge ili aondokane na ulimwengu huu wa mateso ambao alihisi umemtenga baada ya kumtenganisha na wapendwa wake. Akiwa anafungua jokofu na kichukua chupa moja ya konyagi ghafla alishtuka sana. 


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )