Sunday, July 31, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 22 & 23

MTUNZI: ENEA FAIDY

.....MR ALLOYCE alishtuka sana baada ya kusikia kishindo kalikali nyuma yake. Aliachia chupa ya konyagi kisha akageuka haraka kutazama nini kinaendelea nyuma yake. Hakuamini kumuona mwanaye akiwa amejibwaga chini kama gunia la viazi. Alikuwa anathema kupita maelezo.

"Eddy!" Mr Aloyce aliita kwa mshangao mkubwa. Lakini Eddy hakuitikia zaidi ya kuendelea kuhema kwa nguvu.Mr Alloyce alitupa chini vidonge alivyokuwa amevishika, akamwinamia Mwanaye na kumgusa kifuani ili kusikiliza mapigo ya moyo. Aligundua kuwa mwanaye ni mzima alimsgukuru Mungu. Killed home hang a za Mr Alloyce ni kwamba pindi anarudi sebuleni pale, hakukuta mtu yeyote na wala hakusikia mtu akifungua mlango.

"Ba...ba..!" Aliita Eddy kwa shida sana.
"Sema mwanangu...Mimi hapa" aliitikia Mr Aloyce.
"Usife. .!"
"Sifi nani kasema Mimi nakufa? Vipi lakini uko sawa?" Aliuliza mr Alloyce akiwa na hofu sana, alihofia kumpoteza mwanaye kipenzi. Eddy aliitikia kwa kichwa tu akimhakikishia baba yake kuwa yuko sawa.

Mr Alloyce aliendelea kumkagua Mwanaye kila sehemu akidhani labda ana majeraha kwani damu alizozikuta chumbani kwa Eddy zilimtisha Sana. Lakini alipomtazama mwanaye akagundua hana jeraha lolote mwilini mwake, hivyo maswali mengi yalijitokeza akilini mwake. Alijihoji maswali mengi lakini hakuwa na majibu yake.

"Baba... Mama anateseka sana!" Eddy aliongea sauti ndogo ya kujivuta sana akiwa bado amelala pale sakafuni.
"Anateseka wapi?" Mr Alloyce alishtuka sana.
"Alikuja hapa.. Anateseka sana na yote kwa sababu yangu...!" Alisema Eddy kwa huzuni sana huku machozi yakimlengalenga machoni.
"Eddy! Upo sawa kweli?" Mr Alloyce alihisi Eddy hayupo sawa hivyo anaropoka tu anachojisikia.
"Nimefanya makosa sana.. Namtesa mama yangu..."
"Eddy usiseme hivyo.. Unamtesa na nini?"
"Alivyotaka kunipeleka kwa mganga wameamua kumuadhibu...!"
"Kina nani?"
"Wachawi...!"
"Oh My God.."

Maneno Yale yalizidi kumchanganya Mr Alloyce, alishundwa afanyaje kwani ilikuwa ni Mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbana na mauzauza ya namna ile. Mara nyingi alizoea kutazama kwenye luninga tu lakini hakujua kama inaweza kumtokea kweli. Maisha yake yalikuwa machungu ndani ya muda mfupi tu kwanu matatizo aliyokuwanayo yalikuwa mazito tena yanaumiza kama gunia la misumari.
"Baba.. Nakupenda..!"
"Nakupenda pia mwanangu!"

Mr Aloyce alijikuta anashusha mchozi tu kila anapomtazama mwanaye kwanu siku zote aliamini mwanaye atakuwa mtu mkubwa sana kutokana na uwezo wake darasani. Alikuwa na akili nyingi lakini Leo amekuwa mtu wa kuteseka tu. Aliwachukia wanadamu wenzake kwa ukatili wanaoufanya juu ya familia yake.

"Baba.."
"Naam mwanangu.."
"Chukua hii." Eddy alimkabidhi baba yake kipande cha karatasi.Mr Aloyce alishtuka kidogo kisha akapokea karatasi like na kulikunjua ili alisome.Ujumbe uliokuwepo pale ulimshtua sana Mr Alloyce. Aliurudia tena"CHAGUA MOJA.
EDDY APONE TATIZO LAKE, MAMA YAKE APOTEE DAIMA. AU MAMA EDDY ARUDI, EDDY ABAKI NA TATIZO LAKE"

Mr Aloyce alibaki mdomo wazi kwa mshangao, kwani ule ulikuwa mtihani mgumu kwake."Karatasi limetoka wapi?" 

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )