Tuesday, August 9, 2016

AUDIO: Tundu Lissu Amjibu Rais Magufuli

Jumanee ya leo August 9 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam kutoa taarifa kwa umma kuhusu taarifa za vitisho wanazokuwa wakizipata kutoka serikalini.

Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu amesema hakuna mtu toka Chadema anayetaka kumjaribu mtukufu Rais na wala hakuna anayetaka kukamatwa na Polisi  kwa sababu mahabusu sio pazuri.

"Tunachotaka kukifanya ni ambacho kipo katika katiba, mikutano na maandamano ya kisiasa kwakuwa ni halali. Kama kufanya hivyo Rais Magufuli anafikiri tunamjaribu hayo ni mawazo yake" Amesema Tundu Lissu

==> Bofya  Hapo chini kumsikiliza

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )