Saturday, August 13, 2016

Jukwaa la Wahariri lapinga Gazeti la Mseto kufungiwa


 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mwenyekiti wake, Theophil Makunga, TEF imesema, “hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.”


Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.

"Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.

"Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ikaanzisha chombo cha kitaaluma cha kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya kumaliza kadhia hii.

"Serikali imeahidi muda mrefu kubadili Sheria hii mbaya ya Magazeti lakini miaka yote utekelezaji umekuwa sifuri.

"Tunasisitiza kuwa hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.

"Kwa upande mwingine tunapenda kuvitahadharisha vyombo vya Habari katika matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali, Jamii au mtu mmoja mmoja." Amesema Makunga

"Pamoja na taarifa hii, TEF itafanya uchunguzi na uchambuzi wa adhabu iliyotolewa kwa Gazeti la Mseto pamoja na habari iliyosababisha gazeti hilo kufungiwa, kwa manufaa ya waandishi wa habari na vyumba vya habari." Amesema Makunga
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )