Saturday, August 13, 2016

Mwanamke abakwa, auawa na kutupwa kichakani


MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amekufa katika mazingira yanayoonesha kwamba alibakwa kabla ya kuuawa na kutupwa kichakani.

Mwili wake ulionekana Agosti 10, mwaka huu saa 7.30 mchana katika Kijiji cha Iringa Mvumi, Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kwamba wanamfanya msako waliotenda unyama huo ili wawafikishe katika mkondo wa sheria.

Alitoa mwito kwa wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi na vijiji vya jirani kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wahalifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Wakati huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma imemtupa jela miaka 30 mkazi wa Kijiji cha Mlali Iyengu, Mkengela Mchechele (27) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 11.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa, Mary Senapee pamoja na kumtupa jela miaka hiyo, pia aliamuru mtuhumiwa kuchapwa viboko 12 na akitoka jela alipe fidia ya Sh milioni moja.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )