Wednesday, August 24, 2016

Rais Magufuli Amuapisha Mkurugenzi Mkuu Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemuapisha Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Dkt. Modestus Francis Kipilimba ameapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na mara baada ya kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Salome Kaganda.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dkt. Modestus Francis Kipilimba amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika Makungu kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania Bara.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika Makungu alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.

Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimkabidhi kitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.Kushoto akisimamia zoezi hilp ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju na Katibu Mkuu kiongozi Engineer John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.
PICHA ZOTE NA IKULU

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )