Friday, August 12, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 30

Mtunzi:ENEA FAIDY
....Dorice aliendelea Julia huku matone yake ya machozi yakiwa damu. Ghafla akajikuta ana uwezo wa ajabu ambao hajawahi kuufikiria kuwa nao hata siku moja. Alijibadilisha sura na kuwa kiumbe wa kutisha, macho yalikuwa kama ya paka, uso wake ukawa mweusi tii kama mkaa, kucha zake zikawa ndefu sana na meno yake mawili yalichomoza nje ya kinywa chake. Mansoor alicheka kicheko kikali cha kutisha huku sauti ya kicheko chake ikiambatana na mwangwi. Radio zikapiga mfululizo Dorice akatoweka ghafla na kumuacha Mansoor.

Pete aliyokuwa amevalishwa Dorice ilimpa uwezo mkubwa na wa ajabu. Alipata uwezo wa kupotea na kujibadilisha kadri atakavyo lakini sharti kubwa alilotakiwa kufanya ilikuwa ni lazima arudi tena kwa Mansoor baada tu ya kumaliza kazi yake inayompeleka duniani.

Dorice alikuwa ametokeza katika eneo lenye Giza Giza lilitawaliwa sauti za wadudu. Palikuwa na utulivu mkubwa sana , kwani eneo lile halikukaliwa na mtu yeyote zaidi ya ndege, wadudu na wanyama wadogo wadogo. Dorice alibaki anajishangaa, alijiuliza amefika vipi eneo lile akiwa peke yake bila Mansoor.

"Ina maana nimekuwa na nguvu za kijini?" Alijiuliza Dorice. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, Dorice alitazama huku na kule ili kujua nani alikuwa mgeni wake kwa wakati ule. Ghafla Mansoor akajitokeza akiwa anacheka kicheko cha kutisha sana kisha akapiga hatua za taratibu kumsogelea Dorice.

"Kwanini umefika huku?" Aliuliza Mansoor kwa ghadhabu.
"Sijui nimefikaje" alijibu Dorice.
"Muda wako wa kuondoka kwenye himaya yangu bado Dorice, nilikuwa na jaribu kukupa ladha ya vile utakavyokuwa baada ya wakati kutimia" alisema Mansoor.
"Kwahiyo unataka nirudi?"
"Ndio.. Tunarudi wote".

"Hapana Mansoor sitaki kurudi tena Kule" alisema Dorice.
"Ni lazima urudi maana bado sijakupa maelekezo"
"Hayo maelekezo nipe hapa hapa"
"Haraka haraka ilimfanya chura apate ngozi ya mabaka"
"Hata hivyo siwezi kurudi".

Yalizuka mabishano makali baina ya Dorice na Mansoor kwani Dorice hakutaka kurudi kwenye himaya ya Mansoor tena. Alitaka aachwe huru na arudi kwao, lakini mkongwe ni mkongwe tu licha ya mabishano Yale Mansoor aliibuka mshindi baada ya kumchukua Dorice kinguvu kwa kutumia uwezo mkubwa wa kijini alionao. 

Katika eneo walilokuwepo ukatokea upepo mkali na kuwavuta wote wawili kisha ndani ya muda mfupi walijikuta wametokea katika himaya ya akina Mansoor. Dorice alikasirika sana.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )