Friday, August 19, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 23 & 24


 Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
 Mkuu wa shule na akasimama eneo tulilo jificha na Madam Rukia huku kila mmoja akiwa nguo zake amezivaa vizuri baada ya kuwasikia walimu hawa mambao walinitoroka mchana wakizungumza.Mkuu wa shule akaanza kukojoa huku akipiga mluzi akiisikilizia raha ya kukojoa na mkono wake mmoja ameshika bastola yake na gafla Madam Rukia akakohoa na kumfanya mkuu wa shule kugeuka na macho yake na yangu yakakutana huku akionekana kuto amini kuniona katika eneo hili

ENDELEA
Akili yangu ilafanya kazi ya haraka ya kufikiri na wazo lililo nijia ni kumshika Madam Rukia na kumsukuma na akaangukia kwenye miguu ya mkuu wa shule na mimi nikanyanyuka kwa haraka na kuanza kutokomea porini.Milio ya bunduki nikaanza kuisikia kwa nyuma nikajua atakuwa ni mkuu wa shule pamoja na waalimu wengine ambao wanamuunga mkono mkuu wa shule.

Nikafanikiwa kuwaacha kwa umbali mkubwa na kutokana na kuchoka sana ikanilazimu nipande juu ya mti ili niweze kujipunzisha kwani tofauti na hapo ninaweza kupata maumivu makali ya kifua yatokayono na jeraha la risasi nililo kuwa nimepigwa na Manka

Nikajilaz akwenye tawi huku nikiangalia chini na kuumshuhudia mwalimu wa nizamu akipita kwa kasi akielekea nilipokuwa nikielekea.Ndani ya dakika moja wakapita waalimu wengine wawili wakiwa katika mwendo wa kukimbia.Nikaanza kusikia sauti ya Madam Rukia akilia na nikamshugudia mkuu wa shule akiwa amezishika nywele za Madam Rukia huku akimvuta kwa nguvu akimlazimisha atembee kwa haraka

Mkuu wa shule na Madam Rukia wakasimama chini ya mti niliopo huku Madam Rukia akilalamika amechoka
“Nitakuua tambua mimi sasa hivi sio mwalimu wako mkuu.Ohooo wewe niletee ufala”
Mkuu wa shule alizungumza huku bastola yeke akiwa amaiweka kwenye sikio la Madam Rukia la upande wa kushoto.

“Sema huyu fala mwenzako amekwenda wapi?”
“Mimi sijui kwani si alikimbia mbele ya macho yetu”
“Ahaaa hujui eheee?”
“SIJUI MKUU WEWE UNANIONEA TUU”
Mkuu wa shule akavuta kashati ka Madam Rukia na kakachanika na akabaki na sidiria kisha akaanza kumshika shika maziwa kinguvu kiasi kwamba Madam Rukia akaanza kufanya fujo ya kujitoa mikononi mwa mkuu wa shule
“Nitakupasua hichi kichwa”
“Nipasue ila sio kuniambukiza ukimwi wako”
“Ahaaa sasa nakuambukiaza”

Mkuu wa shule akaendelea kuzichana nguo za Madam Rukia kwa kutumia nguvu galfa nikastuka kuiona simu yangu ikienda chini huku ikitoa mwanga na inavyoonyesha inaita na sikujua ni kivipi imetoka mfukoni mwangu na kwabahati mbaya ikaanguka katikati ya Mkuu wa Shule na Madam Rukia.Mkuu wa shule akaiokota simu yangu na kuangalia juu haraka na kuniona.Madam Rukia akampiga mkuu wa shule kigoti cha sehemu za siri na kumfanya atoe ukulele huku akiiangusha simu aliyo ishika.Nikashuka kwenye mti kwa haraka na kumkuta bado mkuu wa shule amejikunja.

Madam Rukia akaiokota simu yangu na mimi nikampiga teke mkuu wa shule lililo tua kwenye kifua chake na kumfanya angukie mgongo kabla sijamsogelea nikwaona waalimu wakirudi katika eneo alilopo mkuu wa shule.Nikamshika mkono Madam Rukia na kuanza kukimbia naye kurudi tulipo liacha gari
“Eddy nimechoka?”
“Jikaze bwana”
“Niache wewe ndenda”
“NINI?”
“Eddy wewe nenda zako mimi niache hapa hapa nitajua cha kufanya”
Nikawaona waalimu wakiwa na mwalimu mkuu wakishuka kwa kasi kwenye kilima wakija katika eneo tulipo

“Eddy wewe nenda na chukua na simu yako”
Mada Rukia alizungumza huku akiwa analia kwa uchungu,Nikaichukua simu nikamuachia mkono taratibu na kuanza kukumbia kwa kasi huku nikianza kuvuta kumbukumbu ni wapi nilipo liacha gari kwani miti mingi iliweza kunichanganya kiasi kwamba nikawa ninazunguka zunguka pasipo kujua ni wapi lilipo gari.Gafla nikasikia mlio wa bunduki na kunifanya nisimame gafla na akili yangu moja kwa moja ikamkumbuka Mada Rukia
“Fuc*k wamemuua”

Nilizungumza huku nikitazama sehemu ulipo tokea mlio wa bunduki,nikataka kurud ila nikasita na kujikuta nikishikwa na bumbuazi.Mwanga wa simu yangu ukanistua na kuigeuza na kukuta namba ngeni ikiingia kwenye simu yangu.Nikaipokea na kujibanza kwenye mti huku nikiwa ninahema kiasi kwamba hata mtu aliye nipigia simu atahisi kitu

“Vipi kijana?’
“Salama nani mwenzangu”
“Mimi ni daktari wa hospiytali uliyo mleta binti wa kike na ukaniachia namba nikujulishe kitakacho endelea”
“Ndiio nimekukumbuka dokta”
“Hali ya Salome sio nzuri nainatubidi yumsafirishe tumpeleke Dar es Salaam kwa matibabu zaidi”
“Kwani tatizo lake lilikuwa ni kubwa sana”
“Ndio mishipa ya damu inayoingiza damu kwenye moyo wake imepasuka”
“MUNGU WANGUUUU”
“Na hapa inabidi sisi kama Hospitali kushuhulika katika garama zote kwa wakati huu ila wewe utakuja kuzilipa”
“Saaaw........Haaaa!!!”

Nikastukia gongo likipiga sehemu ya juu kwenye mti na nikageuka haraka na kumshuhudia mwalimu wa nidhamu ambaye siku zote huwa sipatani naye akija kwa kasi huku akiwa peke yake,Nikaiweka simu yangu mfukoni na kuipandisha juu kidogo suruali yangu ya jeanzi na kumsubiria kwa hamu mwalimu.

Nikastukia mwalimu wa zamu akinipita kwa kasi kama hajaniona na sekunde kadhaa nikaona kundi la vijana wapatao kumi wakija kwa kasi huku wengine wakiwa na mapanga na magongo,
Na mimi nikaungana na mwalimu wa zamu katika kukimbia katika njia anayo elekea huku vijana hao wakionyesha ni wachaga wakitufwata kwa kasi,Tukagawana njia mimi na mwalimu wa zamu kila mmoja akaenda upande anapo pajua yeye huku nyuma yangu wakiwepo vijana wawili wakinifwata mimi

“Mungu wangu nisaidie”
Nilijiesemea kimoyo moyo huku nikijikaza katika kukimbia kiasi kwamba niliaza kuhisi kuchoka huku kifua kikiniuma kwa mbali.Nikakaza mwendao huku nikiwatazama vijana wanao nifwata nikaona wakikata tama ya kunikimbiza na mwisho wa siku wakasimama na kuanza kutukana kilugha na wakarudi walipo tokea.

Nikasimama na huku nikiinama na pumzi nikizihisi zikiniishia pamoja na koo langu kukauka mate.Mazingira ya eneo nililopo yakanipa matumaini kwani ndio sehemu ambayo tulifanyia mapenzi na Madam Rukia,Nikajikaza na kunyanyuka na kwenda lilipo gari na kukuta tairi moja ya mbele ikiwa haina upepo.Nikafungua buti la gari na nakuta batani ikinielekeza niminye nikaminya na ndani ya buti kukafunguka na kukuta tairii  pamoja na vidungu viwili vya lita mbili mbili vya mafuta ya petrol na vinaonekana ni maalumu kwa gari hili kwani bado vina upya
Nikalitoa taira na kuliweka chini huku nikiwa na mashaka na kila muda nikawa na kazi ya kuangalia pande zote za sehemu niliyopo.

Simu yangu ikatoa mwanga ulionekana kwenye mwanga wa jeanzi yangu ikiashiria simu inaita nikaitoa mfukoni na kukuta ni Sheila ndio anapiga nikaipokea na kuibana sikioni kwa kutumia bega
“Baby mbona nilikuwa ninakupigia hupokei?”
“Baby weee acha tu hapa nilipo nipo kwenye matatizo”
“Matatizo gani mume wangu?”
“Wee acha tu nitakusimulia”

“Saa zile nilitaka nikuambie kuwa utazame kuna mafuta ya emergence kwenye buti na sikujua kama ulielewa?”
“Sikuelewa ila sasa hivi ndio ninayaona”
“Fanya basi urudi dady”
“Sawa”
“I love you”
“Love you too”
Nikakata simu na kuirudisha simu ndani ya gari kisha nikaanza kazi ya kufungua tairi lililo na pancha na kulifunga tairi lililo jipya na ikanichukua kama dakika ishirini katika kuikamilisha kazi yangu.

Nikayamimina mafuta kweye tanki la gari kisha nikaingia na kuliwasha na nikazifwata taratibu za uwashaji wa gari hili kisha nikaanza kuomdoka huku nikirudi katika barabara ya niliyo jia.Kutokana ni msituni mingi sikuweza kukimbiza gari kwani ninahofia kuchanganya njia,Gafla nikaona taa za gari zikija mbeke yangu kwa kasi huku zikiwasha king’ora nikatambua watakuwa ni gari la polisi.

Dereva wa gari la polisi akaanza kuliendesa gari lake kwa fujo ya kutanda barabara nzima huku taa zake akiziwasha kwa mtindo wa zima washa kitu kilicho niumiza macho.Nikapungunza mwendo na kadri nilivyojaribu kuwakwepa kwa kubana upande mmoja wa barabara ila dereva wa gari ya polisi akanifwata upande niliopo
“Huyu jamaa ni chizi nini?”

Nilijiuliza kwa sauti ya juu huku gari langu nikilirudisha barabarani ili niweze kuona atanifanya nini.Na yeye akalirudisha barabarani gari lake huku akiziwasha taa zake kwa mtindo ulionikera huku akipunguza mwendo na gari zetu zikabaki zimetazamana huku dereva huyo akivuta akikanyaga mafuta kama wafanyavo madereva wa mashindano ya magari kabla hawajaruhusiwa kuanza kasi.

Nikastuka baada ya kuwaona watu wawili wenye miili mikubwa wakiwa wamevalia makoti meusi na makofia yaliyo yaficha sura zao na kubaki macho wa kishuka kwenye gari ya polisi huku wakiwa na bubduki mikononi wakizielekezea kwangu.Nikairudisha gari nyuma kwa kasi ya ajabu na kuwafanya jamaa kuanza kunishambuli kwa risasi.
‘HALO BWANA EDDY GODWIN GARI YAKO IMEPATA ULINZI BINAFSI’
Sauti ya kike ilisikika kupitia spika zilizopo kwenye gari ambalo kwangu kila kinacho fanyika ninaona ni kipya na sauti hii si ngeni kwangu

‘CHAGUA SILAHA’
Kioo kidogo kilianza kunionyesha aina za bunduki zilizopo ndani ya gari kwa kigugumizi nikajikuta nikijiminyia kwenye silaha ambayo wala sikujua itajitokeza wapi,Gafla gari yangu ikasimama na haikurudi nyuma na nikaanza kusikia mtetemeko ndani ya gari na kuona vitu vyenye moto na vinavyokwenda kwa kasi kali vikitoka sehemu ya mbele ya gari na vikielekea lilipo gari la polisi na kulifanya lirushwe juu na kulipuka huku jamaa wanao nirushia risasi wakianguka chini
“UPO SALAMA BWANA EDDY GODWIN UNAWEZA KUENDELEA NA SAFARI YAKO.ASANTE”

Gari ikarudi katika hali yake ya kawaida na taratibu nikaanza kukanyaga mafuta na kufika katika sehemu ambayo wameangukia watu ambao sikujua lengo lao ni nini hadi wanisambule kwa risasi.

Nikawachungulia kupitia kwenye kioo nikagundua wamefariki kwani miili yao ilijaa matobo mengi yaliyo tokana vichuma vya bomu zilizo toka kwenye gari huku damu nyingi zikivuja kwenye miili yao,Nikashuka huku nikitetemeka na kuanza kumfunua mmoja baada ya mwengine na kujikuta kumbukumbu zangu zikirudi hadi siku niliyo kamatwa pamoja na derava wetu na kuingizwa katika maabusu ya kituo cha polisi Lushoto na kulikuwa na majaamaa yenye misuli mikubwa na katika mazungumzo yetu walisema wao ni majambazi sugu wanashuhulika na utekaji wa magari.

Sura mbili za majamaa wale ndizo zilizo lala chini,Sikutaka ushahidi nikaingia haraka ndani ya gari na kuondoka katika eneo hili.Baada ya lisaa nikawa nimefika mjini na muda ulio timu sasa ni saa kumi na nusu usiku.

Nikafika hospitalini na kulisimamisha gari katika maengesho ya magari nikatoa simu yangu mfukoni na kuakuta missed call nyingi za Sheila.Nikafumba macho yangu na kusali kwa kumshukuru Mungu kunisaidia kutoka katika majanga yaliyo nikuta ila nafsi na moyo wangu vikajikuta vikiniuma kutokana na kifo cha madam Rukia
Nikashuka ndani ya gari na kwenda moja kwa moja katika chuma alicholazwa Sheila ila sikumkuta na nikatoa simu na kumpigia akapokea nesi

“Mgonjwa wangu yupo wapi?”
“Tumemuhamisha chumba panda huku gorofani ukunje kushoto chumba namba 16 ndipo alipo mgonjwa wako”
“Sawa”
Nikafanya kama alivyonielekeza nesi na kuingia katika chumba namba 16 na kumkuta Sheila akiwa hana raha na baada ya kuniona akataka kushuka kitandani kuja kunikumbatia ila sindano ya dripu ilimzuia,Nikamfwata na kumkumbatia na sote tukajikuta tukitokwa na machozi ya furaha

“Mume wangu pole”
“Asante mke wangu”
“Mimi kidogo hali yangu inaendele vizuri zile sindano walizo nichoma kidogo kidonda kimeanza kukauka kwa haraka”
“Nijambo la kumshukuru Mungu”
Nikaanza kumuadisia Sheila yaliyo nikuta ila sikumuadisia juu ya Madam Rukia kwani ninajua nilicho kitenda hakikustahili kwa mimi kumfanyia
“Sasa huyo uliye mgonga anaendeleaje?”
“Sijajua ila asubuhi itanibidi nikamfwatilie niweze kujua ni nani?” 

==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )