Monday, August 22, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 25 & 26 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


 Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

 
Ilipoishia...
Nikambusu sheila mdomoni na kufungua mlango na kutoka na moja kwa moja nikashuka hadi kwenye chumba alicho nielekeza  sheila.Nikagonga mlango mara tatu na suti ya kike iliyopo ndani ya chumba hicho ikaniruhusu niingie.

Nikafungua mlango na kuwakuta manesi watatu wakiwa wameshika mashavu yao huku wakionekana wanyongea na macho yao wameyaelekezea kwenye kioo cha tv iliyopo ndani ya chumba hicho.

Na mimi ikanibidi ninagalie wanacho kitazama na kukuta mipigo ya moyo yakiende kwa kasi baada ya kuiona ndege kubwa ikiwa imeanguka huku inawaka moto na kutoa moshi mwingi na mweusi huku kikosi cha zima moto ambacho sikujua ni cha nchi gani wakijitahidi kuzima moto kwa kutumia magari yao maalumu ya kuzimia moto huku baadhi ya miili inayoonekana kuwa imefariki ikitolewa ndani ya ndege hiyo

Endelea...
“karibu kaka yangu tukusaidie nini?”
Nesi mmoja aliniuliza swali ila sikumjibu nikabaki nikiitazama taarifa inayorushwa kupitia kituo cha televishion ya sky news kinachopatikana nchini uingereza.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio kana kwamba nimekimbia umbali mrefu pasipo kupumzika.Nikayasoma maandishi makubwa yaliopo ubavuni mwa ndege hiyo na kukuta yameandikwa emirates kiasi kwamba nikajikuta nikishusha pumzi taratibu na manesi wote wakabaki wakinitazama.

“kaka kaka”
“naam”
“mbona unashangaa?”
“ninatazama hiyo taarifa ya habari”
“inasikitisha sana kwa maana watu wote waliopo kwenye hiyo ndege wamefariki”
“imekuwaje hiyo ndege ikaanguka?”
“ilianguaka kipindi inapaa imesababishwa na hali ya hewa kutokuwa nzuri”
“imeangukia nchi gani?”
“imeangukia tailand”

Kidogo nafsi yangu ikapata unafuu na tabasanu likarudi usoni mwangu taratabu kwani nilidhani itakuwa ni ndege ambayo amepanda mama.Nikawaomba dawa za kutuliza maumivu ya kichwa wakanipatia pamoja na maji nikazinywa na kuwashukuru na kuondoka na kuwaacha wakiendelea na shughuli zao.Nikaenda kwenye maduka ya simu ambayo hayakuwa mbali sana na hopsitali na kununua simu kwa ajili ya sheila na kupitia kwenye sehemu wanapouza chipisi.Nikanunua chips za kutosha na kurudi hospitali na kumkuta sheila akizungumza na madaktari.
“hali yako inazidi kuridhisha na baada ya siku kadhaa tunaweza kukupa ruhusa ya kutoka hospitali”

“kwani hamuwezi kunipata hata leo?”

“kwa leo ni vigumu inabidi umalizie dozi yako ya vidonge na sindano za kukausha kidonda na baada ya hapo tutakuwa huru katika kukuruhusu.”

Tukakaa hospitalini siku mbili huku nikiendelea kumuuguza sheila na ndani ya siku mbili sikuweza kupata taarifa yoyote kuhusiana na mama juu ya kupatikana kwa ndege yao ambayo imetekwa na watu wasio julikana.Sheila akaruhusiwa kutoka hospitalini na akapewa vidonge ambavyo endapo atajisikia maumivu ameze.Nikapepeleka gari gereji kufanyiwa ukarabati wa vitu vidogo vidogo na kumuacha sheila akijiandaa kwa ajili ya safari ya kurudi dar es salaam.

“kaka hii gari umeinunua wapi?”
“kwa nini?”

“nina mwaka wa 21 tangu nianze kutengeneza magari ila sijawahi kuiona gari ya dizain hii kwa maana mmmm imekusanya mambo mengi”
“ahaaa hizi gari mbona zipo ukihitaji unazipata tuu”
“aise ila hii gari si chini ya milioni mia na kitu”
“imezidi zaidi ya hapo”

Niliendelea kuzungumza na fundi mkuu wa gareji ambayo nimeileta gari yangu,nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma nikageuka na kukutana na sura ya madam rukia na kunifanya nistuke kiasi kwamba mapigo ya moyo yakaaza kunienda mbio.

“mbona unastuka eddy?”
“ha.....Pana nimeshangaa tu kukuona hapa”
“wife(mke) unajuananaye huyo kijana?”
Fundi gereji aliuliza swali na kujikuta nikizidi kupata kigugumizi chakuzumza kiasi kwamba nikaabaki nimekaa kimya

“ndio ni mwanafunzi wangu wa kidato cha tano,huyo ndio chanzo cha shele yetu kufungiwa”
“kaka sura yako inaonyesha mpole kumbe ni mkorofi kiasi hicho?”

“hapana mambo ya kawaida”
Nilizungumza huku nikibabaika kwani kila nikimtazama madam rukia ninakumbuka tukio lililotokea porini na jinsi nilivyo fanya naye mapenzi kwenye kichaka isitoshe nikakumbuka niliusikia mlio wa bunduki na kujua ni lazima atakuwa ameuawa na mkuu wa shule.

“ehee lete story edy ile siku ilikuwaje?”
Madam rukia aliniuliza swali baada ya mume wake kuondoka na kuingia kwenye moja ya chumba na kuanza kuzungumza  na wafanyakazi wake.Nikamuadisia madam rukia kuanzia tulipo achana hadi nikafika hopsitalini na yeye akaanza kuniadisia tangu tulipo achana.

“mimi ile siku bwana nilikutana na vijana ambao ni wanakijiji cha karibu kwenye ule msitu wenyewe walikuwa wanakwenda kuwinda.....Sasa pale ulipo niacha mkuu wa shule na wezake si wakawa wananifwata basi wale vijana wakatanda ile sehemu tuliyopo na kuanza kuwashambulia waalimu na kuwatoa mbio za kufa mtu basi ikawa ndio pona pona yangu”

“mbona nilisikia mlio wa bunduki alipigwa nani?”
“ahh mkuu wa shule si alikuwa anajifanya kidume anapiga bastola juu hewani ili kuwatisha wale vijana......Wee alipigwa gongo moja la pua hata sijui ile bastola aliitupia wapi nilisikia akitoa ukulele wa uwii na kuanza kukimbia....Sasa na ile miguu yake yenye matege ya kaekejea upande mmoja ungekuwepo ungecheka”

“mmmm sasa ulirudije mjini?”
“wale vijana wakaniazimisha simu na nikampigia my husband(mume wangu) nikamuelekeza nilipo akaja kunichukua na tukarudi mjini pamoja”
“ulimuambia jamaa kuhusiana na jinsi ulivyo fika porini?”

“ndio ila nilimuambia kuna majambazi ndio waliniteke...Ehee madam merry anaendelea vizuri amefanyiwa upasuaji na kizazi chake kimerekebishwa vizuri ila sasa hivi yupo powa”

Madam rukia alibadilisha mada baada ya mume wake kufika katika eneo tulilopo na sikuwa na haja ya kujiuliza ni kwanini amebadilisha mada nikajua moja kwa moja ahitaji mumu wake atambue kuwa mimi nilikuwa naye porini

“hivi wamesemaje kuhusiana na swala zima la shule kuendelea?”

“wamesema watatoa tangazo kwenye vyomba vya habari pele shule itakapo funguliwa ila kwa sasa wameunda tume ya madai yaliyopelekea shule kufungwa ambayo itachunguza kila kitu na wanafunzi walio kamatwa na polisi wapo wengine wanahojiwa”

“sasa hiyo tume watatumia muda gani kuchunguza hayo madai yato kwa maana siku zinakwenda mbele na masomo ndio hivyo yamesimama?”

“mimi wala sielewi ila kidato cha sita na cha nne wamesambazwa kwenye shule za jirani ili kuendelea na masomo hadi pale majengo yatakapo fanyiwa ukarabati nao ndio watarudi”
“ahaaa....”
“wewe sasa hivi unakwenda wapi dar au kwa marry?”
“huyo merry mimi wala sihiaji kumsikia kwa maana mume wake amenizingu sana majuzi”
“wee amekuonea wapi?”
“si nilikwenda kumcheki hospitalini sasa nikawakuta wana mazungumzo yao basi mimi ikanibidi niwaache niondoke zao basi jamaa akanifwata na kuanza kunipiga vibao mbele za watu na mimi nikampiga basi mambo yakaharibika pale hospitali nikaamua kumpotezea”

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )