Tuesday, August 2, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 5 & 6


 Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
 “Samahani kaka sijui wewe ni nani mwenzangu?”
“Unaniuliza mimi ni nani ndani ya nyumba yangu?”
Moyo ukanipiga paaaa kama jiwe lililotua juu ya bati tena la nyumba ya uswahilini.Nikajua jamaa anaweza akawa mume wa Madam Mery mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio pale jamaa alipoanza kupiga hatua za kwenda chumbani kwa Madam Mery kwani boxer na tisheti ya shule vyote vipo ndani ya chumba hicho na vipo sehemu ya wazi kwa mtu yoyote anayeingia lazima ataviona,na kingine kilichozidi kunipagawisha ni kitanda nilivyo kiacha kimevurugika kwani kinaonyesha hivi hivi kilikuwa ni kiwanja cha mechi za wakubwa

ENDELEA
    Jamaa kabla hajafunua pazia ili aingie ndani simu yake ikaita.Akaitoa kwenye mfuko wa suruali kisha akaipokea na kuanza kuzungumza mazungumzo ambayo yalianza na ndio bosi.Jamaa akanitazama kisha akatoka nje nikahisi mazungumzo yake ni muhimu sana na ya siri sana ndio maana akatoka nje huku begi lake akilivua na kuliweka pembeni ya mlango wa kuingilia chumbani kwa Madam Mery.

Ikawa nafasi kwangu kuingia chumbani nikachukua kila kilicho changu huku shuka lililo changungaka nikilitoa na kulisokomeza mvunguni mwa kitanda na kuliacha godoro likiwa na foronya yake tu pasipo kuwa na shuka,Nikarudi hadi sebleni na kumuona jamaa akirudi ndani kwani mlango aliuacha wazi kidogo.Ikanibidi boxer yangu niiweke mfukoni mwa suruali yangu huku tishet yangu nikiwa nimeishika mkononi huku nikitaka kuivaa

“Dogo unakwenda wapi?”
“Ehee”
”Hujasikia…! Unakwenda wapi?”
“Kununua vitafunio vya chai”
“Dogo mbona unajifanya mjanja sana?”
Maswali ya jamaa yakazidi kunichanganya akili na kunizidisia presha ambayo sikuelewa kama inapanda au inashuka.
“Mjanja wa nini brother?”
“Huendi kununua vitafunio ila sema ninakwenda kununua vitafunwa kwani vitafunio ni hayo meno yako”
“Sawa bro nimekuelewa”
“Ehee kwanza hujaniambia wewe ni nani? Nakuona upo upo tu humu ndani?”

“Mimi ninaitwa Eddy”
“Yuko wapi Mery?”
Nkaanza kufikiria cha kumjibu huku maswali mengine nikijiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe ndani ya moyo wangu hadi nikapata muafaka wa nijibu nini
“Amelazwa kwenye hospitali ya shule”
“Lini?”
“Leo asubuhi”
Lengo la kumjibu jamaa kiufasaha kila swali analo niuliza ni ili akienda kumuangalia Madam Mery iwe nafasi ya mimi kuondoka katika nyumba hiyo ili nikatafute hata sehemu ya kuishi nikisubiria siku zangu za kusimamishwa masomo ziishe

“Powa dogo vaa tisheti yako unipeleke huku alipolazwa”
Sikuwa na ujanja zaidi ya kuivaa tisheti yangu na kumalizia kuvaa viatu vyangu na kitu kilichozidi kuniweka mpole mbele ya jamaa ni pale alipoitoa bastola yake na kutazama kama inarisasi za kutosha kwenye magazine yake na kuirudisha kiunoni bastola yake huku akionekena kuridhika na risasi zilizomo.

Safari ikaanza huku sote tukiwa kimya ila mimi nimetangulia mbele kama hatua moja huku yeye akifwatia kwa nyuma.Akili yangu ikawa inanituma nipige hatua za haraka haraka na kama kuna uwezekano nikimbie kwani vichochoro vyote ninavijua katika mji huu wa Arusha
“Dogo nasikia kuna majambazi sana wamezuka kipindi cha hivi karibuni?”

“Kusema ukweli bro mimi mwenyewe ninasikia sikia ila sina uhakika kivile.Ila ni juzi kuna benki pale mbele ilivamiwa na pesa zote zikaibiwa”
“Dogo subiri ninunue P.K hapa dukani si utakula?”
“Ndio”

Jamaa akaingia kwenye moja ya duka,nikamchungulia kwenye duka hilo nikamuona yupo bize na muuza duka.Nikaanza kupiga hatua za taratibu huku nikizuga zuga watu waliopo katika eneo hilo wasistukie kitu chochote ili nikifika mbali na duka hilo nianze kukimbia.Kabla sijafika mbali kidogo gafla nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma.Nikageuka na kukutana na muuza mahindi
“Oya broo yule jamaa pale mjeda ameniambia nikuletee maindi uchague”

Nikatamani nimtukane muuzaji wa watu ila nikaona hana kosa taratibu nikaanza kuyatazama mahindi yaliyo chomekwa kwenye spoke za baiskeli zipatazo kumi na kuunganishwa katika mti mmoja.Nikachagua muhindi laini laini kwani sikuwa nimekula kitu cha aina yoyote tangu asubuhi.Jamaa akaja hadi tulipo akatoa noti ya elfu kumi na kumpa muuza maindi na kumuambia chenchi akae nayo
“Aisee kamanda wangu Mungu akubariki sana”

Muuza maidi alizungumza kwa lafudhi ya kichaga huku akipiga saluti na kumfanya jamaa acheke ila mimi sikuwa na hata hamu ya kuyakenua meno yangu.Tukaendelea na safari ya kwenda katika hospitali ya shule ambayo haikuwa mbali sana na shule kwani ilikuwa pia inatoa msaada wa kuwahudumia wananchi wa kawaida tofauti na wanafunzi

Tukafika hospitalini na tukakutana na Madam Rukia akiwa nje ya wodi ya wagonjwa,nikamsalimia nikabaki nikiwatazama jinsi  anavyo salimiana na jamaa huku wakicheka kwa furaha na kuonekana wakifahamiana kwa muda mrefu
“Huyo mwenzako anaendeleaje?”
“Kidogo joto lake limeshuka kwani asubuhi hali yake haikuwa nzuri kivile”
“Tatizo lake ni nini haswa?”

“Maleria alikutwa na vidudu sita ndio vimemlaza.”
“Sasa mbona umekaa huku nje?”
“Nilitoka mara moja kupunga punga hewa ila twende ukamuone”
Wakati wote wanazungumza nilikuwa kimya nimetulia kama maji ya mtungini huku moyoni nikifurahia jamaa aingie ndani na mimi niondoke .Jamaa na Madam Rukia wakaanza kuingia ila jamaa akasimama na kuniangalia
“Oya dogo twende ukamuangalie mgonjwa”

“Huyu mwalifu umemtoa wapi?”
Madam Rukia alimuuliza jamaa na kumfanya atabasamu ila kwangu nikazidi kuogopa,cha kumshukuru Mungu jamaa hakulijibu swali la Madam Rukia kwani tayari tulishafika ndani ya chumba alicholazwa Madam Mery.Jamaa akakaa kitandani na kumkumbatia madam na wote kwa pamoja wakawa wanatokwa na machozi ya furaha,sikujua kinacho waliza ni nini

Wakaachiana huku jamaa akianza kumfuta Madam Mery machozi kwa kutumia kitambaa chake na kunifanya roho yangu kuanza kuhisi maumivu ya wivu 

==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )