Wednesday, August 3, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 7 & 8


MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA....

Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio na kujikuta nikianza kuomba sala ya kuniepusha na kukamatwa kwetu kwani ni muda mchache ulio pita baba alitoka kunionya kwa ujinga kama huo.Nikamtazama Salome na taratibu nikamuona mwenzangu akilegea kabla hajaanguka nikamuwahi kumkumbatia ili asianguke chini na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.......

ENDELEA....

.....Nikaendelea kumshikilia Salome ambaye anahema Kwa pumzi za taratibu kutokana na giza sikujua kama ameyafumba macho yake.Mlango ukatingishwa kidogo kama mtu anayetaka kufungua na kuingia.

“Eddy…..Eddy”

Nikasikia ni sauti ya chini ya John ikiniita nje ya mlango, Nikawa na wasiwasi huenda atakuwa yupo na walinzi au mwalimu ili iwe rahisi kwa kunikamata endapo nitaitiaka.Akarudia kuniita tena ila nikakausha kimya nikamsikia akiendelea kufungua fungua vyoo vingine na baada ya muda sikumsikia tena.

“Salome Salo”

Nilimuita Salome huku nikimtingisha taratibu ila mwenzangu hakunijibu kitu chochote.Nikakumbuka baba alinipa simu nikaitoa mfukoni na kuiwasha nikammulika Salome nikakuta mwenzangu macho yake yamebadilika na kiini cheusi cha katikati ya jicho sikukiona na kulifanya jicho lake lote kuwa jeupe.Mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku taratibu nikahisi umotomoto kwenye mapaja yangu na kuifanya suruali yangu kulowana nikajua moja kwa moja mtu mzima nimeshalimwaga mbele ya Salome ambaye sielewi amepatwa na nini.

Kwa jinsi miguu inavyotetemeka nikashindwa kuizuia hali ya kulimwaga kojo ambalo linachuruzika kwenye mapaja kwa kasi huku likiwa la motomoto na mbaya zaidi nimetoka kuchimba mgodi muda si mrefu na sikufikia mwisho wa uchimbaji.Kwa uzito wa Salome na kukosa kwangu muhimili wa kusimama nikajikuta nikianza kushuka chini taratibu huku mgongo ukiwa unaburuzika ukutani hadi nikakaa chini.  

Nikaendelea kumnong’oneza Salome ila mwenzangu hakuitika sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumkumbatia huku kichwa chake akiwa amekilaza juu ya kifua changu,cha kumshukuru Mungu ni vyoo tulivyopo hakuna hata kimoja ambacho kimetumika kwani ndio kwanza vipya vinamsubiria diwani aje kuvizindua siku mili mbeleni.

Nikaanza kumlaani John kwa masihara yake nikahisi kwamba alikuja kunitania na utani wake umweniachia majanga ambayo sijui niyamalize vipi kwani hata kusimama ninashindwa kwa jinsi suruali yangu ilivyolowana na mbaya zaidi mwili mzima unanitetemeka

Nikatazama saa ya kwenye simu nikakuta ni saa tano kasoro usiku,nikaendelea kusubiri huku mara kwa mara nikiwa ninamtingisha Salome ili azinduke.Baada ya masaa mawili kupita huku nikiwa nipo macho gafla Salome akapiga chafya nikaiwasha simu na kummulika Salome usoni nikakuta anaanza kufumbua fumbua macho na matumaini ya kutokulala chooni yakaanza kunijia kwani nilishakata tama nikajua ni lazima nitalala chooni.

“Salome”
“Mmmm”
“Unajisikiaje”
“Mmmmm”
“Unajisikiaje….?”
“Kidogo afadhali”
“Unaweza kusimama?”
“Mwili hauna nguvu”

Ikanilazimu kusubiri ili Salome nguvu ziweze kumrudia.Masaa yakazidi kukatika huku kila nikimuuliza Salome juu ya kurejewa na nguvu anadai bado.Nikaanza kupata wasiwasi kwani hadi sasa hivi imesha timu saa tisa usiku.Kijimwanga kikaanza kuchomoza na kuingia katika uwazi wa chini katika choo.Nikashangaa Salome akikurupuka na kusimama kama mtu aliyekuwa akiota ndoto mbaya

“Eddy tupo wapi?’
“Chooni”
“Tupo chooni Eddy…..bwenini kwetu hawajachukuliwa rollcal?” 


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )